Friday, September 10, 2010
   
Text Size

Tafuta kwenye Website hii

Mtikila kwenda jela miezi 6

MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala imemhukumu Mchungaji Christopha Mtikila kutumikia kifungo cha madai cha miezi sita baada kushindwa kumlipa fedha zake, Bi. Paskazia Matete.

Akitoa hukumu hiyo Hakimu Mfawidhi, Bi. Joyce Minde alisema hukumu hiyo itaanza pale tu mdai, Bi. Matete atakapolipia sh. 100,000 kila mwezi za kumhudumia mdai atakapokuwa gerezani.

"Mtikila ataanza kutumikia kifungo mara tu mdai atakapowasilisha fedha za kumhudumia katika matatizo mbalimbali likiwemo chakula," alisema Hakimu Minde

Mdai anatakiwa kutoa fedha taslimu sh.100,000 kila mwezi ambapo kwa kipindi cha miezi sita atakachokua gerezani mchungaji huyo atatoa sh. 600,000.

Bi. Minde amesema kutokana na sheria hiyo mdaiwa akitumikia kifungo hicho hatatakiwa kulipa deni analodaiwa.

Alisema Bi. Matete akitaka kulipwa deni lake anaweza kukamata mali za Mtikila anazozifahamu ili ziuzwe kufidia deni, na endapo mali hizo zitakamatwa Mtikila hatatumikia kifungo hicho.

Katika kesi hiyo Mtikila na mwenzake Bi. Mariam Isaa wanadaiwa kumkopa Bi. Matete sh. milioni 9 lakini walishindwa kumlipa.

Hukumu hiyo ilitolewa Mahakamani bila ya Mchungaji Mtikila kuwepo mahakamani.

CHANZO MAJIRA

Comments
Add New Search
pett22  - kesi ya mtikila   |80.84.1.xxx |2010-07-30 07:51:44
mbona hii kesi haieleweki yaan nakudai then ufungwe mm niwenakulisha huko
gerezani semeni mtikila kashinda kesi sio kafungwa kesi alafu alishwe na raia
uliona wapi basi tungefungwa wengi au nikiwahuko gerezani naagiza chakula
ninachotaka?
Write comment
Name:
Email:
 
Title:
UBBCode:
[b] [i] [u] [url] [quote] [code] [img] 
 
 
Please input the anti-spam code that you can read in the image.

3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."

Login Form