Eriksson kutofundisha Ivory Coast
Chama cha Soka cha Ivory Coast tayari kimesema walifanya mazungumzo na kocha huyo wa zamani wa England kwa ajili ya kuijaza nafasi hiyo.
Kocha huyo raia wa Sweden alikutana na viongozi wa Ivory Coast wiki iliyopita lakini hakuna makubaliano yaliyofikiwa.
Wakala wake Athole Still amesema "Sidhani kama Eriksson anahitaji kazi hiyo ya kuifundisha Ivory Coast. Natumai hatafundisha soka wakati huo wa Kombe la Dunia".
Wakala huyo alithibitisha walikutana na viongozi wa soka wa Ivory Coast, lakini walikwenda kuangalia mechi waliyocheza na Korea Kusini na kukutana na viongozi tu hakuna jingine.
Ivory Coast kwa sasa inamuwinda Mholanzi Guus Hiddink kuinoa timu yao kwa ajili ya Kombe la Dunia mwezi Juni nchini Afrika Kusini.
| Comments |
|

