Pienaar afungiwa kuendesha gari
Kiungo huyo wa Everton alitolewa ndani ya gari na polisi wa Merseyside alfajiri ya tarehe 21 mwezi wa Februari baada timu yake kuichapa manchester United mabao 3-1 .
Mchezaji huyo raia wa Afrika Kusini alikutwa amekunywa pombe kwa kiwango cha mara mbili zaidi ya kiwango kinachokubalika wakati alipofanyiwa kipimo cha pumzi na polisi wa Liverpool.
Pienaar, mwenye umri wa miaka 27 alipigwa faini ya paundi 1,000 za Uingereza na mahakama ya Liverpool.
Pia ametakiwa kulipa faini nyingine zaidi ya paundi 100 kutokana na kushindwa kufuata sheria za barabarani.
| Comments |
|
Powered by !JoomlaComment 3.26

