Saturday, July 31, 2010
   
Text Size

Tafuta kwenye Website hii

Twiga yaikung'uta Ethiopia 3-1

Timu ya taifa ya soka ya wanawake ya Tanzania, Twiga Stars imeifunga timu ya taifa ya Ethiopia kwa mabao matatu kwa moja.

Mchezo huo umefanyika mjini Addis Ababa.

Mwenyekiti wa chama cha soka cha wanawake nchini Tanzania, Lina Mhando amekiambia kipindi cha Michezo na Wachezaji cha BBC kuwa goli la kwanza limefungwa na Esther Chamburuma.

Amesema bao la pili limefungwa na Mwanahamisi Omari la tatu kufungwa na Asha Rashid.

Timu hizo zitakutana tena wiki mbili zijazo, katika mechi itakayochezwa mjini Dar es Salaam.

Atakayeibuka mshindi baada ya mechi hizo mbili atacheza na Eritrea, kufuatia timu ya Kenya kuamua kujiondoa katika mechi hizo za kufuzu.

Comments
Add New Search
Write comment
Name:
Email:
 
Title:
UBBCode:
[b] [i] [u] [url] [quote] [code] [img] 
 
 
Please input the anti-spam code that you can read in the image.

3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."

Login Form