Rafa siendi Juve
Kocha wa Liverpool Rafa Banitez ameendela kusisitiza kuwa yeye hana mpango wa kujiunga na klabu ya serial A ya italia Juventus mwishoni mwa msimu mwa ligi.
Tetesi tuko huko nchini Italy zimesema vigogo hao wa nchini humo, ambao wiki iliyipita walimuajiri bwana Alberto Zaccheroni kuwa kocha wao wa muda wamekubaliana na matakwa ya kocha huyo wa Liverpool na mjumbe alikuwa akilekea Merseyside leo kujaribu kuongea na viongozi wa Liverpool.
Lakini Banitez alisema "naema hili ili watu wote mjue na hasa kwa vyombo vya habari vya Italia sina makubaliano yoyote na juventus na sina mpango wa kuonana na wawakilishi wao au klabu yoyoyte nyengine ile, kwa sababu nina mkataba wa muda mrefu na Liverpool na ninafuraha kuwepo kwenye klabu hii"
Ninachokifikiria sasa hivi ni kazi yangu na kuirudisha timu kwenye nne bora, nikianzia na mchezo wa jumamosi dhidi ya Everton.
| Comments |
|

