Sisi sio timu ya mtu mmoja
Mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney, ambaye mpaka sasa ndiye anayeongoza kwa upachikaji magoli kwenye ligi kuu ya Uingereza jana usiku alisisitizakuwa "sisi sio imu ya mtu mmoja"
Rooney alifikisha magoli 21 juzi siku ya jumatano baada ya kufunga goli la ushindi na kuipeleka timu yake kwenye fainali za carling cup ambayo itakutana na Aston Villa kwenye dimba la Wembley.
Bila kujali upachikaji wake wa mabao kwa msimu huu na juhudi anazozionesha akiwa uwanjani alisisitiza kwa kusema "msituangalie sisi kama kama timu ya mtu mmoja, au muione kama mzigo kwangu, hiyo haileti maana. Kama sitapata ushirikiano kutoka kwa wenzagu na kama hawata nipatia huduma nzuri basi nisngeweza kufunga magoli, wote tumechangia kupata magoli hayo, na timu ndio inayoshinda sio mtu binafsi" alimalizia kwa kusema Rooney.
| Comments |
|

