Friday, September 10, 2010
   
Text Size

Tafuta kwenye Website hii

Wahariri kujadili jinsi ya kuwasaidia wapiga kura wakati wa kampeni

Wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini watakutana jijini Dar es salaam kesho kujadili mikakati ya kuwasaidia wapiga kura wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani mwaka huu, ili waweze kuwahoji wagombea watafanya nini katika kutatua kero zao.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake nchini (Tamwa), Ananilea Nkya, katika taarifa iliyoyolewa kwa vyombo vya habari jana jijini Dar es Salaam.

Katika taarifa hiyo, Nkya, alisema kuwa miongoni mwa kero kubwa zinazorudisha nyuma maendeleo ya wananchi hasa wanawake ni mfumo usioridhisha wa elimu ambao unachangia idadi kubwa ya wanafunzi kutopata elimu bora na kuwepo kwa ongezeko kubwa la mimba shuleni.

Aliitaja kero nyingine sugu kuwa ni idadi kubwa ya vifo vya wanawake vinavyoweza kuzuilika vinavyotokana na ujauzito kwani hivi sasa wanawake zaidi ya 26 hufariki dunia kila siku hapa nchini kutokana na matatizo yanayoweza kuzuilika iwapo huduma za afya zitaboreshwa.

Tatizo jingine kubwa linalokabili wanawake na wanaume wengi alisema ni kipato duni ambapo kwa njia moja au nyingine huchangia kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya ukimwi na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Mkutano huo utakaofanyika katika ofisi za Tamwa, Sinza Mori, jijini Dar es Salaam, kuanzia saa 4:00 asubuhi ambapo wahariri watajadili pia umuhimu wa wapiga kura kupambana na rushwa kwenye uchaguzi ili taifa liweze kupata viongozi makini na waadilifu kuharakisha maendeleo ya wananchi.

Tafiti zinaonesha kuwa rushwa kwenye uchaguzi ndicho chanzo kikubwa cha taifa kupata viongozi waroho, wanaojilimbikizia mali, wasiokuwa na uwezo na nia ya dhati ya kuwatumikia wananchi na taifa lao.


CHANZO: NIPASHE
Comments
Add New Search
Write comment
Name:
Email:
 
Title:
UBBCode:
[b] [i] [u] [url] [quote] [code] [img] 
 
 
Please input the anti-spam code that you can read in the image.

3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."

Habari Motomoto

  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20

Login Form