Mwalimu aliyefariki aendelea `kula` mshahara, apanda cheo
Halmashauri ya wilaya ya Bunda, imeingia kwenye kashfa kubwa baada ya kubainika kumlipa mshahara mwalimu aliyekufa mwaka 2007.
Aidha, mwalimu huyo pia alipandishwa daraja mwaka 2009 na mshahara wake haijulikani unachukuliwa na nani .
Kashfa hiyo iliyoibuliwa juzi kwenye kikao cha kawaida cha baraza la madiwani na kuwaacha wajumbe wakiwa wameduwaa, inazidi kuonyesha wazi kuwa tume iliyopita kuhakiki watumishi hewa haikufanya kazi kama ilivyotarajiwa.
Akizungumza katika kikao hicho, diwani wa Kata ya Kibara, Venance Kamonyore, alisema anashangazwa na kitendo cha ofisi ya
Mkurugenzi kuendelea kupokea mshahara wa marehemu mwalimu Charles Mwijarubi aliyekuwa akifundisha katika Shule ya Msingi Namibu, Kata ya Kibara ambaye alikufa mwaka 2007.
“Niliwahi kumuuliza Mkurugenzi inakuwaje mtu amekufa mwaka 2007 mshahara wake unaendelea kuja mpaka sasa, la kushangaza mwaka 2009, alipandishwa daraja na mshahara kuongezeka...ndugu zake wanataka kujua nani anachukua fedha zao,” alihoji diwani.
Alisema ndugu zake walikuwa tayari kwenda wizarani kudai fedha hizo na ufisadi wa kutumia jina la marehemu kujipatia fedha ambazo familia yake hazijazipata.
“Toka nimeongea na Ded, sijapata majibu. Hivi kweli fedha hizo zinarudishwa Hazina na kwa nini jina hilo liendelee kuonekana kama yuko kazini wakati alishafariki dunia sasa ni mwaka wa nne,” alizidi kuhoji.
Hoja hiyo iliyosisimua baraza ilimfanya Mkurugenzi Mtendaji, Cyprian Oyier, kujitutumua kuijibu, akikiri kuwa aliambiwa na diwani na kufuatilia ili jina hilo liondolewe na mshahara usije.
“Nilimweleza ahakikishe wanawaandikia Hazina jina hilo liondolewe, yuko hapa atajibu kama mshahara huo unakwenda wapi, maana kama jina halijaondolewa utaendelea kuja,”alisema Mkurugenzi.
Hata hivyo Kaimu Mweka Hazina, Stella Msangya, hakuweza kujibu tuhuma hiyo mpaka mwisho wa kikao hali ambayo inazidisha mashaka juu ya tuhuma hiyo iliyoibuliwa ghafla.
Kaka wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina moja la mwalimu mstaafu Wijarubi, akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu alisema wao wanafuatilia kuona ufisadi huo wa kutumia majina ya marehemu kupata fedha.
Alidai kuwa mpaka risti za mishahara ya Januari, mwaka huu ipo na wanayo na kuwa mrithi wa mali za marehemu ambaye ni kijana wake, James Mwijarubi, alimfikia diwani Februari, mwaka huu baada ya kupata taarifa na katika ufuatiliaji walibaini ukweli wa mambo.
Baadhi ya madiwani walisikitishwa na mchezo huo ambao walidai ni kashfa kubwa kwa halmashauri huku wakidai kuwa tume zinazoundwa kuchunguza watumishi hewa hazijazaa matunda kwa kuwa majina hewa bado yapo sekta za elimu na afya.
| Comments |
|
3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."
Habari Motomoto
-
Mahakama: Chenge ana kesi ya kujibu Mahakama ya wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam imesema mgombea...
-
Vyama 15 vyasaini rasimu ya mwongozo wa maadili Z`bar Viongozi wa vyama 15 vya siasa jana walisaini rasimu ya mwongozo...
-
Mrufani aongezewa adhabu ya viboko Mahakama ya rufaa Tanzania imemuongea adhabu Mathias Mhagama, aliyepinga...
-
Tanesco yalalamikia vituo bandia vya Luku Shirika la Umeme nchini (Tanesco) limesema kuna ongezeko la vituo...
-
Chadema: Hatutaki siasa za maji taka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema hakina muda...
-
CCM na Chadema Moshi jino kwa jino Mkutano kati ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Lucas Ng’hoboko...
-
Tendwa aiduwaza Chadema Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, ametupilia mbali pingamizi...
-
Chagueni viongozi pasipo kuangalia vyama-Mdee Mgombea ubunge wa jimbo la Kawe kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo...
-
Wanawake wanaougua akili wananyanyasika Wanawake wanaougua ugonjwa wa akili, wananyanyasika kutokana na...
-
Slaa, Dk Bilal uso kwa uso Mwanza Mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),...
-
Mtihani darasa la saba wafanyika kwa utulivu Mtihani wa darasa la saba ulioanza jana kote nchini, ulifanyika katika...
-
Vurugu zaibuka Moshi, Iringa Watu watano wamekamatwa na Polisi mkoani hapa, wakihusishwa na vurugu...
-
Takukuru yapigwa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), imezidi kubanwa...
- 1
- 2
- 3
- 4
- 5
- 6
- 7
- 8
- 9
- 10
- 11
- 12
- 13
- 14
- 15
- 16
- 17
- 18
- 19
- 20
Zilizosomwa Sana
- Schorlaships
- MAJINA YA WANAFUNZI 33658 WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO, VYUO VYA UFUNDI NA CHUO CHA MAJI MWAKA 2010
- United States
- CHAKULA CHA USIKU: WAHANGA SASA NI WANAWAKE! - Mwambie, usione haya
- Dawa za Kuongeza Ufanisi wa Mwanaume Kitandani Zazinduliwa
- AFYA! AFYA! Mambo yote muhimu haya hapa
- Europe
- ***BREAKING NEWS: Watuhumiwa wote kesi ya ZOMBE waachiliwa huru!!!***
- Advertisement Plan
- Australia
- Aliyefumwa akibaka bintiye ala kichapo
- Man Utd ushindi sasa basi
- Ratiba ya Ligi Kuu Uingereza 2010/2011
- Chanjo ya HIV yapunguza maambukizi
- Wanafunzi walioteketea kuzikwa kaburi moja leo
- Japan

