RCO atoa ushahidi kesi ya wizi NMB
Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa kipolisi wa Ilala (RCO), Duani Nyanda (49), ametoa ushahidi wake katika kesi ya wizi wa zaidi ya Sh. milioni 234 mali ya benki ya NMB tawi la Mwanga mkoani Kilimanjaro na kueleza jinsi walivyoweza kuwatia mbaroni washtakiwa watano.
Nyanda ambaye ni shahidi wa 18, alikuwa akitoa ushahidi wake jana mbele ya jopo la mahakimu watatu, Penterine Kente, Aziza Temu na John Nkwabi wanaosikiliza kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi.
Akiongozwa na wakili wa serikali Kanda ya Arusha, Juma Ramadhani, alidai kuwa mnamo Julai 11 mwaka 2007 alipata taarifa kuwa kuna majambazi wamevamia benki hiyo.
Alidai kuwa aliitwa na mkuu wake wa kazi kwa wakati huo, Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Alfred Tibaigana, ambaye alimtaka kuungana na askari wengine kwa ajili ya kufanya upelelezi wa tukio hilo.
Alidai baada ya kufika aliungana na askari wa upelelezi wa Wilaya ya Mwanga na Moshi na kuanza upelelezi ambapo simu ya mmoja wa mtu aliyeuwawa na polisi kwa kupigwa risasi akidhaniwa ni jambazi raia wa Kenya, Peter Mbungua, ndio iliwawezesha kuwapata baadhi ya washtakiwa.
Alidai katika simu hiyo waliangalia mtu aliyewasiliana na marehemu mara ya mwisho na kukuta ni mtu aitwaye Brenda, mkazi wa Arusha, ambapo waliomba kukutana naye.
Alidai kuwa Brenda aliwaeleza polisi kuwa alifahamiana na marehemu huyo kupitia mshtakiwa wa 11, Juliana Musanza, ambaye alimsaidia kupata simu ya kiganjani, ambapo walikwenda nyumbani kwake Julai 20, mwaka 2007.
Alidai baada ya kufika nyumbani kwa mshtakiwa wa 11, waliwakuta mshtakiwa, Devota Musanza ambapo katika kuwahoji waliwapeleka mahali wanapoishi mshtakiwa wa kwanza na wa pili katika eneo la Njiro mkoani Arusha.
Shahidi huyo aliendelea kudai kuwa baada ya kufika katika nyumba hiyo majira ya usiku waliizingira hadi saa 12 alfajiri ndipo alipoaanza kuishambulia kwa kuwataka washtakiwa hao wajisalimishe.
Alidai washtakiwa hao walianza mashambulizi baada ya kushtuka kuwa polisi wamezingira nyumba hiyo na kulazimika kuomba msaada wa askari zaidi kwa kikosi cha Arusha.
Alidai walipambana na washtakiwa hao baada ya kurusha mabomu ya machozi na risasi, ambapo mshtakiwa Elizabeth alijisamilisha na kueleza kuwa ndani ya nyumba hiyo kuna watu wengine wawili.
Alidai walifanikiwa kuwakamata mshtakiwa wa kwanza, Samwel Saitoti na wa pili, Peter Kimani, ambapo baada ya kuwapekua waliwakuta wamevaa nguo za kuzuia risasi, silaha ya za kivita mbili aina ya SMG moja ikiwa na risasi 50 na nyingine risasi 26.
Pia alidai kuwa walikutwa na bastola 5 na mshtakiwa wa kwanza alikuwa na dola za Kimarekani 8,145 huku mshtakiwa wa pili akiwa na sh milioni 1.7.
Kesi hiyo inaendeleo leo ambapo shahidi huyo anaendelea kutoa ushahidi wake.
| Comments |
|
3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."
Habari Motomoto
-
Wahariri kujadili jinsi ya kuwasaidia wapiga kura wakati wa kampeni Wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini watakutana jijini...
-
Slaa apata mapokezi makubwa Musoma, Mwanza Maelfu ya wananchi, wakiwamo watumishi wa serikali, wafanyabiashara...
-
Jaji Mkuu: Hatukushinikizwa hukumu ya mgombea binafsi Jaji Mkuu wa Tanzania, Augustine Ramadhan, amesema uamuzi wa Mahakama...
-
Ajali ya basi yaua abiria 16 Watu 16 wamefariki dunia na wengine 48 kujeruhiwa baada ya basi la...
-
Kura ya maoni Z`bar yamg`oa DC Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, amemfukuza kazi Mkuu wa Wilaya...
-
Takukuru sasa inatawala nchi Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imewakamata makada...
-
Karume awa mbogo Z`bar Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume, amevunja ukimya kwa kusema kuwa...
-
Umati wamlaki Slaa jijini Arusha Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod...
-
Jaji Eliamani Mbise afariki dunia Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Eliamani Mbise, amefariki dunia...
-
Tume ya uchaguzi yataka ushahidi wizi wa kura Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeomba kupewa taarifa za mianya ya wizi...
-
Waibuka washindi Viti Maalum CCM Wagombea kadha wameibuka na ushindi katika mchuano wa kura za uteuzi...
-
Waziri Sitta azungumzia sakata ya Takukuru Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Magreth Sitta, amekanusha...
-
Kamanda Takukuru ashushwa cheo WAKATI habari za rushwa zikiendelea kutawala harakati za kuwania ...
- 1
- 2
- 3
- 4
- 5
- 6
- 7
- 8
- 9
- 10
- 11
- 12
- 13
- 14
- 15
- 16
- 17
- 18
- 19
- 20
Zilizosomwa Sana
- Schorlaships
- MAJINA YA WANAFUNZI 33658 WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO, VYUO VYA UFUNDI NA CHUO CHA MAJI MWAKA 2010
- United States
- CHAKULA CHA USIKU: WAHANGA SASA NI WANAWAKE! - Mwambie, usione haya
- AFYA! AFYA! Mambo yote muhimu haya hapa
- Dawa za Kuongeza Ufanisi wa Mwanaume Kitandani Zazinduliwa
- Europe
- Advertisement Plan
- ***BREAKING NEWS: Watuhumiwa wote kesi ya ZOMBE waachiliwa huru!!!***
- Aliyefumwa akibaka bintiye ala kichapo
- Australia
- Man Utd ushindi sasa basi
- Wanafunzi walioteketea kuzikwa kaburi moja leo
- Chanjo ya HIV yapunguza maambukizi
- United Kingdom
- Henry Joseph Shindika aula

