Ngeleja: Serikali kununua Dowans ndoto
Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, amekanusha vikali kwamba serikali imelegeza msimamo wake wa kukataa kununua mitambo ya kufua umeme ya Kampuni ya Dowans Tanzania Limited na sasa iko katika mchakato wa kuinunua.
Hivi karibuni uliibuka uvumi kuwa serikali imeamua kuinunua mitambo hiyo licha ya kusitisha mipango hiyo baada ya shinikizo la Bunge mwaka jana.
Akizungumza na gazeti hili jana jijini Dar es Salaam, Waziri Ngeleja alisema kuwa taarifa hizo si za kweli kwani msimamo wa serikali ni kutoinunua mitambo hiyo yenye uwezo wa kufua umeme wa megawati 100.
“Unajua hayo ni maneno tu ya mitaani labda ndio wanadhani kuwa serikali itanunua mitambo ya Dowans, ila napenda kuwahakikishia wananchi kuwa serikali haipo kwenye mchakato huo kama wanavyofikiria,” alisema Waziri Ngeleja.
Moja ya maazimio ya Bunge katika mkutano wake wa Februari mwaka 2008 ni kuitaka serikali kuvunja mkataba na Dowans, ambayo ilirithi mkataba wa kuzalisha umeme wa dharura kutoka kwa kampuni tata ya Richmond Development (LLC) ambayo ilibainika kupata zabuni hiyo kinyume cha sheria na taratibu.
Vile vile uchunguzi uliofanywa na Kamati Teule ya Bunge iliyoongozwa na Mbunge wa Kyela (CCM), Dk. Harrison Mwakyembe, kuichunguza Richmond nje na ndani ya Tanzania ulibainisha kuwa ilikuwa kampuni ya kitapeli.
Baada ya kubainika kuwa serikali iliipa zabuni hiyo kwa njia za upendeleo, aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na mawaziri wawili walioiongoza Wizara ya Nishati na Madini kwa nyakati tofauti, Dk. Ibrahim Msabaha na Nazir Karamagi walilazimika kujiuzulu. Kabla serikali haijatangaza nia yake ya kutoinunua mitambo hiyo, ulizuka mjadala mkubwa uliowahusisha wabunge, maofisa wa serikali, wanasiasa na makundi mbalimbali ya jamii huku kundi moja likitaka inunuliwe na lingine likipinga.
Hoja kwamba serikali imebadili nia kuhusu mitambo ya Dowans ilitiwa nguvu na habari zilizozagaa mitaani hivi karibuni na kuripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari kwamba zabuni ya ununuzi wa majereta ya kuzalisha umeme wa magewati 160 imesitishwa kwa kuwa sasa mchakato ni kununua Dowans.
Serikali ilisimamisha mchakato wa zabuni uliokuwa umefikiwa na Tanesco, na kutoa siku 90 kwa ajili ya kupitiwa kwa taratibu zite za zabuni kwa mujibu wa sheria ya manunuzi ya umma.
Serikali ilichukua uamuzi huo baada ya kugundua kulikuwa na ukiukaji wa taratibu kama zilivyoanishwa kwenye sheria ya manunuzi ya umma. Kwa hili hiyo, Waziri Ngeleja alisema zabuni hiyo sasa itafunguliwa Machi 19, mwaka huu (Ijumaa ya wiki ijayo).
Wakati huo huo, Waziri Ngeleja jana alisaini mkataba wa makubaliano baina ya wizara yake na Kamati Tekelezi Tasnia ya Uziduaji (EITI).
Alisema kuwa lengo la taasisi hiyo ni kuendeleza na kudumisha uwajibikaji na uwazi wa utoaji wa taarifa kuhusu mapato yanayotokana na uvunaji wa rasilimali za madini. Aidha, alisema EITI ni taasisi itakayosimamia utekelezaji wa programu na taratibu zinazotambulika kimataifa katika kuweka uwazi wa mapato ya uvunaji wa rasilimali za madini, gesi asilia na mafuta kwa umma.
Alisema suala hilo litasaidia kuwawezesha wananchi kufahamu mchango wa rasilimali hizo katika maendeleo ya nchi.
“Suala ni kwamba wananchi watapatiwa taarifa sahihi za mchango wa uwekezaji katika rasilimali za nchi na hivyo kujenga imani kwa serikali katika kuwaletea maendeleo endelevu kupitia taasisi hiyo,” alisema Ngeleja. Kwa mujibu wa Ngeleja, serikali ipo kwenye mchakato wa kuhakikisha makundi ya kijamii pamoja na makampuni yanahusika katika kuunda kamati tekelezi ya EITI yenye wajumbe 15 watakaosimamia suala hilo.
Ngeleja alisema utekelezaji wa shughuli hizo unahitaji ushirikishwaji wa jamii, makampuni na ngazi mbalimbali katika serikali ili kuhakikisha maendeleo ya nchi yanapatikana kupitia rasilimali hizo.
Aliongeza kuwa serikali inatambua umuhimu wa kuwepo kwa sheria itakayosimamia shughuli za Tasnia ya Uziduaji na kwamba hivyo inakusudia kuanzisha mchakato wa utungaji wa sheria hiyo.
Aidha alisema taasisi hiyo tayari imeshaanza kazi, ila kwa sasa wapo kwenye mchakato wa kuandaa muswaada ili upelekwe bungeni katika mkutano ujao.
Alisema asilimia 45 ya mapato ya nchi hutokana na madini, hivyo taasisi hiyo itasaidia kuongeza uwazi wa upatikanaji wa matumizi hayo katika rasilimali ya nchi.
Mwenyekiti wa Tasnia ya Uziduaji, Jaji Mstaafu Mark Bomani, aliahidi kuwa taasisi hiyo itafanya kazi kwa uwazi na uadilifu ili rasilimali za nchi zinufaishe taifa pamoja na wawekezaji.
Muswada wa kuruhusu kura ya maoni wakamilika
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imesema muswada wa sheria ya kuruhusu kura ya maoni kwa wananchi wa Zanzibar kabla ya kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (GNU) tayari umekamilika.
Hayo yameelezwa na Naibu Msaidizi Mwanasheria Mkuu, Saleh Said Mubarak, alipokuwa akizungumza na Nipashe, kuhusu matayarisho ya sheria hiyo kabla ya kuwasilishwa katika kikao cha Baraza la Wawakilishi na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Kiongozi, Hamza Hassan Juma.
Alisema sheria hiyo ndio itakayoweka utaratibu wa kura ya maoni inayotarajiwa kufanyika kabla ya uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Alisema Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) ndiyo iliyopewa mamlaka ya kuitisha na kusimamia kura ya maoni kulingana na sheria na kanuni zitakazotungwa baada ya kupitishwa kwa sheria hiyo.
Aidha, alisema suala la elimu ya uraia kuhusu kura ya maoni litapangiwa muda wake na NEC, kwa kuzingatia kanuni zitakazotungwa baada ya kupitishwa kwa sheria hiyo.
Alisema utekelezaji wa masuala yote yanayohusu kura ya maoni yamewekewa ratiba maalum ili kuhakikisha mambo yote yanakwenda kama yalivyopangwa bila ya kuathiri uchaguzi mkuu.
Naye Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Ibrahim Mzee, alisema muswada wa kuipa mamlaka ZEC, kuitisha kura ya maoni kabla ya kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa utawasilishwa katika kikao cha Machi 24, mwaka huu.
| Comments |
|
3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."
Habari Motomoto
-
Wahariri kujadili jinsi ya kuwasaidia wapiga kura wakati wa kampeni Wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini watakutana jijini...
-
Slaa apata mapokezi makubwa Musoma, Mwanza Maelfu ya wananchi, wakiwamo watumishi wa serikali, wafanyabiashara...
-
Jaji Mkuu: Hatukushinikizwa hukumu ya mgombea binafsi Jaji Mkuu wa Tanzania, Augustine Ramadhan, amesema uamuzi wa Mahakama...
-
Ajali ya basi yaua abiria 16 Watu 16 wamefariki dunia na wengine 48 kujeruhiwa baada ya basi la...
-
Kura ya maoni Z`bar yamg`oa DC Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, amemfukuza kazi Mkuu wa Wilaya...
-
Takukuru sasa inatawala nchi Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imewakamata makada...
-
Karume awa mbogo Z`bar Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume, amevunja ukimya kwa kusema kuwa...
-
Umati wamlaki Slaa jijini Arusha Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod...
-
Jaji Eliamani Mbise afariki dunia Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Eliamani Mbise, amefariki dunia...
-
Tume ya uchaguzi yataka ushahidi wizi wa kura Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeomba kupewa taarifa za mianya ya wizi...
-
Waibuka washindi Viti Maalum CCM Wagombea kadha wameibuka na ushindi katika mchuano wa kura za uteuzi...
-
Waziri Sitta azungumzia sakata ya Takukuru Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Magreth Sitta, amekanusha...
-
Kamanda Takukuru ashushwa cheo WAKATI habari za rushwa zikiendelea kutawala harakati za kuwania ...
- 1
- 2
- 3
- 4
- 5
- 6
- 7
- 8
- 9
- 10
- 11
- 12
- 13
- 14
- 15
- 16
- 17
- 18
- 19
- 20
Zilizosomwa Sana
- Schorlaships
- MAJINA YA WANAFUNZI 33658 WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO, VYUO VYA UFUNDI NA CHUO CHA MAJI MWAKA 2010
- United States
- CHAKULA CHA USIKU: WAHANGA SASA NI WANAWAKE! - Mwambie, usione haya
- AFYA! AFYA! Mambo yote muhimu haya hapa
- Dawa za Kuongeza Ufanisi wa Mwanaume Kitandani Zazinduliwa
- Europe
- Advertisement Plan
- ***BREAKING NEWS: Watuhumiwa wote kesi ya ZOMBE waachiliwa huru!!!***
- Aliyefumwa akibaka bintiye ala kichapo
- Australia
- Man Utd ushindi sasa basi
- Wanafunzi walioteketea kuzikwa kaburi moja leo
- Chanjo ya HIV yapunguza maambukizi
- United Kingdom
- Henry Joseph Shindika aula

