Jaji Bomani kutopambana na Rais Kikwete 2010
BAADA ya kutajwa kuwa na dhamira ya kumvaa Rais Jakaya Kikwete, kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba kupitia CCCM, Mwanasheria Mkuu wa zamani, Jaji Mark Bomani, amevunja ukimya na kusema hajafikiria kugombea kiti hicho; bali ataendelea kuikosoa serikali.
Kauli hiyo Jaji Bomani ambaye ni mmoja wa watu wanaoheshimika nchini kutokana na historia yake ya kuutumikia mfumo wa uongozi wa nchi kuanzia awamu ya kwanza, imetolewa wakati kuna wingu zito ndani ya CCM kuhusu watu wanaotaka urais.
Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalumu jijini Dar es Salaam jana, Jaji Boma alibainisha: Tena hili naomba uniquote (uni nukuu) vizuri, sina mpango wa kugombea urais 2010.
Hadi sasa watu wanaotajwa ndani ya CCM kuwa na dhamira ya kumvaa Rais Kikwete ni pamoja na swahiba wake Edward Lowassa, Waziri Mkuu mstaafu Dk Salim Ahmed Salim, Profesa Mark Mwandosya Spika wa Bunge wa Samuel Sitta huku John Shibuda akiwa tayari ameweka bayana msimamo wake wa kugombea kiti hicho kwa tiketi ya chama hicho tawala.
Lowassa mwenyewe pia amewahi kunukiliwa akisema hana mpango huo, kwani Rais Kikwete ni rafiki yake huku Profesa Mwandosya, Spika Sitta na Dk Salim wakiwa kimya hadi sasa hivi.
akitoa kauli hiyo ya kwanza tangu ahusishwe na mbio hizo za kuusaka urais wa 2010, Jaji Bomani alisema: "Kuna mambo mengi, kwanza umri, mtu unapaswa kujiuliza kabla ya kuwa na dhamira kwamba je, umri wangu huu naweza kubeba mzigo wa urais?"
Mwanasheria huyo aliyebobea katika fani na mmoja wa wazee wanaoheshimika nchini, alisema umri ni moja ya kigezo cha msingi kwa mtu anayefikiria kuutaka urais. "Mimi umri umepita, alisisitiza Jaji Bomani.
Alipoulizwa kwamba, inadaiwa kuwa amekuwa na mpango wa kumzuia Rais Kikwete asigombee ili yeye achukue nafasi hiyo na kuunda serikali ya mpito; alicheka na kujibu kwa msisitizo: " Hakuna kitu kama hicho nakwambia".
Hata hivyo, Jaji Bomani hakusita kuweka msimamo wake akisema ataendelea kuwa mkosoaji na msimamizi wa misingi na miiko ya uongozi ambayo ilijengwa na waasisi katika taifa.
"Ninachoweza kusema ni kwamba, nitaendelea kukosoa kwa hoja mambo yote yanayohusu uongozi wa nchi hili. Hilo lazima tuliseme na mambo ya nchi yanapaswa kujadiliwa kwa uwazi hata kama watu hawataki," alisema Jaji Bomani.
Alifafanua kwamba, kuna mambo mengi ambayo nchi imefanya makosa katika kulinda misingi na rasilimali za taifa, ikiwemo madini kitu ambacho hadi sasa kimefanya uchumi kuwa duni na umasikini wa Watanzania kuongezeka.
Jaji Bomani ambaye alikuwa mwenyekiti wa Tume ya Rais kuhusu upitiaji wa Sheria ya Madini na namna nchi inavyoweza kunufaika na rasilimali hiyo, alisema sheria ya mwaka 1998 imetumbikiza nchi katika umasikini kutokana na kushindwa kutumia vyanzo hivyo vya uchumi kujiendeleza.
Jaji Boman alitoa mfano kuwa mwaka 1998 pauni moja ya madini ya dhahabu ilikuwa ni dola za Marekani 260, lakini sasa hivi imepanda hadi takriban dola 1,400.
Alifafanua kwamba, anashangaa hadi sasa kosa hilo bado linaendelea wakati uchumi wa nchi unahitaji kiasi kikubwa cha mapato ya madini kwa ajili ya kupunguza umasikini.
Jaji Bomani alisisitiza kuwa sheria hiyo pia inampa fursa mwekezaji katika sekta ya madini kuweka fedha zake za mauzo kwenye benki za nje ya nchi, kitu ambacho kingefanywa kwa nchini hata thamani ya shilingi ingeweza kukua kwa kasi.
Alisema ndiyo maana katika kamati yake, walipendekeza asilimia 60 ya fedha za kigeni za mauzo ya madini nje, ikiwemo dhahabu ziwekezwe kwenye benki za hapanchini ili mzunguuko wake unufaishe nchi.
"Ikiwa asilimia 60 ya fedha za madini kama dhahabu zikiwekwa kwenye benki za ndani ya nchini, ikiwemo Benki Kuu (BoT), ni wazi zitaongeza uimara wa shilingi yetu na hata benki zinaweza kuzitumia katika mizunguuko yao ya fedha" alifafanua na kuongeza:
"Benki zipo hapa hata za kimataifa, sijui tatizo ni nini? Tumezembea hapa kati kati, yaani hatujaweza kutumia vema fursa za utajiri wa kitaifa. Leo hii fedha zote za mauzo ya madini ikiwemo dhahabu kutoka migodi mikubwa ziko nje ya nchi".
Jaji Bomani aliongeza kwamba, madini ni sehemu ya mfano unaonyesha nchi imeshindwa kutumia vema maliasili zake katika kuondoa umasikini na kukuza uchumi na kutaka mkazo maalumu.
"Yapo maeneo mengi, kuna mambo ya utalii na maeneo mengi ya uchumi bado hatujaweza kujipanga vizuri haya lazima tuyaseme kwa uwazi hata kama watu hawataki, na mimi nitasema," aliongeza.
Hivi karibuni Jaji Bomani alishangaa serikali kupinga mgombea binafsi katika uchaguzi akisema kuwa haina sababu ya kuogopa kwa vile hiyo ni njia moja wapo ya kukuza demokrasi nchini.
Alikumbusha kuwa kuwa na mgombea binafsi haimaanishi wagombea binafsi katika nafasi mbalimbali watashinda, kwani historia inaonyesha kuwa katika nchi zilizoruhusu mfumo huo wanakabiliwa na ushindani mkali na asilimia kubwa hawashindi.
CHANZO MWANANCHI
| Comments |
|
3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."
Habari Motomoto
-
Wahariri kujadili jinsi ya kuwasaidia wapiga kura wakati wa kampeni Wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini watakutana jijini...
-
Slaa apata mapokezi makubwa Musoma, Mwanza Maelfu ya wananchi, wakiwamo watumishi wa serikali, wafanyabiashara...
-
Jaji Mkuu: Hatukushinikizwa hukumu ya mgombea binafsi Jaji Mkuu wa Tanzania, Augustine Ramadhan, amesema uamuzi wa Mahakama...
-
Ajali ya basi yaua abiria 16 Watu 16 wamefariki dunia na wengine 48 kujeruhiwa baada ya basi la...
-
Kura ya maoni Z`bar yamg`oa DC Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, amemfukuza kazi Mkuu wa Wilaya...
-
Takukuru sasa inatawala nchi Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imewakamata makada...
-
Karume awa mbogo Z`bar Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume, amevunja ukimya kwa kusema kuwa...
-
Umati wamlaki Slaa jijini Arusha Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod...
-
Jaji Eliamani Mbise afariki dunia Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Eliamani Mbise, amefariki dunia...
-
Tume ya uchaguzi yataka ushahidi wizi wa kura Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeomba kupewa taarifa za mianya ya wizi...
-
Waibuka washindi Viti Maalum CCM Wagombea kadha wameibuka na ushindi katika mchuano wa kura za uteuzi...
-
Waziri Sitta azungumzia sakata ya Takukuru Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Magreth Sitta, amekanusha...
-
Kamanda Takukuru ashushwa cheo WAKATI habari za rushwa zikiendelea kutawala harakati za kuwania ...
- 1
- 2
- 3
- 4
- 5
- 6
- 7
- 8
- 9
- 10
- 11
- 12
- 13
- 14
- 15
- 16
- 17
- 18
- 19
- 20
Zilizosomwa Sana
- Schorlaships
- MAJINA YA WANAFUNZI 33658 WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO, VYUO VYA UFUNDI NA CHUO CHA MAJI MWAKA 2010
- United States
- CHAKULA CHA USIKU: WAHANGA SASA NI WANAWAKE! - Mwambie, usione haya
- AFYA! AFYA! Mambo yote muhimu haya hapa
- Dawa za Kuongeza Ufanisi wa Mwanaume Kitandani Zazinduliwa
- Europe
- Advertisement Plan
- ***BREAKING NEWS: Watuhumiwa wote kesi ya ZOMBE waachiliwa huru!!!***
- Aliyefumwa akibaka bintiye ala kichapo
- Australia
- Man Utd ushindi sasa basi
- Wanafunzi walioteketea kuzikwa kaburi moja leo
- Chanjo ya HIV yapunguza maambukizi
- United Kingdom
- Henry Joseph Shindika aula

