Saturday, July 31, 2010
   
Text Size

Tafuta kwenye Website hii

Kapuya, Tucta washangaana

SERIKALI imesema inafanya uchunguzi kujua sababu zilizofanya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (Tucta) kumshutuma Rais Jakaya Kikwete kwamba hashughulikii malalamiko ya wafanyakazi wanayompelekea.

Jumatatu wiki hii Katibu Mkuu wa Tucta, Nicholas Mgaya alimtuhumu Rais Kikwete kwamba hashughulikii matatizo yao licha ya kupelekewa mara kadhaa; hivyo wakaahidi kuwa hawatamwalika kwenye sherehe za wafanyakazi mwaka huu, kama mgeni rasmi na badala yake rais wa shirikisho hilo ndiye atakayepewa heshima hiyo.

Akizungumza na Mwananchi jana, Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Profesa Juma Kapuya alisema hadi jana ofisi yake haikuwa na taarifa juu ya msukumo ulioihamasisha Tucta hadi kutoa kauli nzito namna hiyo.

Kutokana na mazingira hayo, Profesa Kapuya alisema wizara yake inafanya uchunguzi kuhusiana na suala hilo na hasa kujua kiini cha mhamasiko huo ambao unaelekea kuwashutua wengi.

"Mimi bado sijapata kwa undani juu ya taarifa hizo (za Tucta). Nilikuwa safarini, ndio kwanza narejea. Lakini ofisi yangu inafutailia ili kujua suala hilo kwa undani. Tunataka kujua chanzo ni nini," alisema Profesa Kapuya.

Tamko la Tucta limemshangaza waziri huyo mwenye dhamana ya wafanyakazi nchini na hadi akasema haamini kwamba, Rais Kikwete amekuwa akipuuzia matatizo ya wafanyakazi nchini.

"Rais Kikwete amekuwa karibu sana na wafanyakazi. Amekuwa hata akitenga muda wa kuzungumza nao. Sasa ukiniambia hawajali wafanyakazi, hili linanishangaza," alisema Profesa Kapuya.

Licha ya kumtetea rais, Profesa Kapuya alielezea kuwa wizara yake; ambayo husimamia na kushughulikia matatizo ya wafanyakazi kwa niaba ya Rais Kikwete, imekuwa ikifanya kila jitihada kutatua matatizo ya wafanyakazi.

"Wizara imejitahidi kushirikiana na vyama vya wafanyakazi pamoja na waajiri ili kuboresha maslahi ya wafanyakazi... Kwa kipindi kifupi tu tumeshughulikia zaidi ya kesi 16,000 za wafanyakazi," alisema Profesa Kapuya.

Profesa Kapuya alitoa maelezo hayo siku mbili baada ya Tucta kutoa tamko kuwa haitamualika Rais Kikwete wala kiongozi yeyote wa serikali katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani mwaka huu na badala yake rais Tucta, Ayubu Omary ndiye atakuwa mgeni rasmi.

Mgaya pia alisema, Rais Kikwete alishindwa kuweka wazi kitu kilichobainishwa na tume ya Ntukamanzima aliyoiunda mwaka 2007 kuchunguza matatizo ya wafanyakazi, licha ya tume hiyo kuumia mamilioni ya fedha za walipakodi.

Hatuelewi kwanini Rais Kikwete amefanya ripoti ya tume hii kuwa siri, tunaamini ndani yake kuna mambo ambayo yatatusaidia, alisema Mgaya na kuongeza:

Tumekuwa tukimualika kila mwaka, lakini hana msada wowote kwetu; kwa hiyo sasa hutuna sababu ya kumualika mtu ambaye hatusaidii, alisisitiza Mgaya.

Katika hatua nyingine Mkufunzi wa Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA) ambaye pia ni Mweyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu, Sayansi, Teknolojia, Habari na Utafiti (Raawu), Profesa Kiko Hamza, alisema imefika wakati Watanzania wajue kutafuta haki zao na siyo kusubiri serikali iwaletee.

Profesa Hamza alisema, matatizo yaliyopo nchini sasa yametokana na Watanzania kuwachangua viongozi ambao hawakusitahili kuchaguliwa.

Hakuna Sababu ya kuchagua mtua au chama ambacho hakikusaidii, huu utakuwa mwaka wa masilai, alisema Profesa Hamza.

Profesa Hamza ambaye aliwataka wafanyakazi wote nchini kuungana na kudai haki zao, alisema Tanzania ina kila kitu, hakuna sababu ya wananchi wake kuwa masikini.

Hata hivyo, jana jioni kupitiua Naibu Katibu Mkuu wa wake Nicholaus Mgaya, Tucta imesema kuwa imeshangazwa na kauli ya Kapuya kudai serikali inashirikiana na wafanyakazi kutatua kero zao huku akieleza kuwa jambo hilo siyo kweli na limewafanya wasiwe na imani na serikali.

Mgaya alisema kila mwaka Tucta imekuwa ikilalamika kuhusu nyongeza ya mishahara, kodi kubwa na malipo makubwa ya hifadhi ya jamii, lakini mpaka sasa hakuna hata suala moja ambalo limepatiwa ufumbuzi.

Alisema ripoti iliyotolewa mwaka juzi na wajumbe waliounda kwa ajili ya kufikisha mapendekzo ya nyongeza ya mishahara imekuwa siri hadi lini wakati wafanyakazi wanaumia katika hai ngumu ya maisha.

Alisema kitendo cha Waziri Kapuya kudai wanashirikiana siyo la kweli, kwa sababu mwaka 2009 katika bodi ya mishahara ambayo ilimaliza muda wake Aprili alishindwa kuteua wajumbe, na kuifanya Tucta kuwa na mashaka katika suala zima la utatuzi wa matatizo na malalamiko yao.

Tunamshangaa Waziri kwa sababu mpaka sasa ameshindwa kuteua wajumbe wapya katika bodi ya mishahara, hiyo ndiyo ingekuwa chachu ya kutusaidia katika kupeleka maombi yetu, leo anasema tunashirikiana na matatizo yetu wanayashughulikia, ni yapi? Mbona hata mapendekezo ya nyongeza ya mishahara wameshindwa kuyafanyia kazi?, alisema Mgaya akihoji.

Alibainisha kwamba, kutokana na hali hiyo, Tucta imefikia uamuzi huo baada ya kuona kuwa Rais Jakaya Kikwete ameshindwa kutekeleza ahadi ya kuwasaidia wafanyakazi, jambo ambalo linawakosesha imani, na kuamua kuingia katika maamuzi mazito kama hayo.

CHANZO MWANANCHI

Comments
Add New Search
sisty  - Kapuya,TUCTA washangaana.   |196.43.79.xxx |2010-03-11 04:24:23
Enyi wafanyakazi wazalendo wa Tanzania,hii si karne tena ya kupewa ahadi
hewa.Wanasiasa wanachoangalia ni maslahi yao kwanza,walala hoi baadae.
Write comment
Name:
Email:
 
Title:
UBBCode:
[b] [i] [u] [url] [quote] [code] [img] 
 
 
Please input the anti-spam code that you can read in the image.

3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."

Habari Motomoto

  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20

Login Form