Watu 3,000 wapiga simu kujua kama Maalim Seif amekufa
ZAIDI ya watu 3,800 wamepiga simu kutoka kona mbalimbali duniani kwa viongozi mbalimbali wa Chama cha Wananchi (CUF), wakitaka kufahamu kama kuna ukweli wowote kwamba Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharrif Hamad, alikuwa amefariki duni au la.
Maalim Seif alilazwa Hospitali ya Hindu Mandal iliyo jijini Dar es Salaam tangu Ijumaa iliyopita, baada ya kuugua ghafla ugonjwa wa mkamba (bronchitis), ambao unatokana na kuvimba kwa njia za hewa, baada ya mapafu kushambuliwa na vijidudu.
Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na Mwananchi, jumla ya simu 3,885, zilipokelewa juzi na viongozi saba wa ngazi za juu wa CUF kutoka kwa watu mbalimbali wakitaka kufahamu kama kweli Maalim Seif amefariki dunia au la.
Wakizungumza na Mwananchi kwa nyakati tofauti viongozi hao walisema, simu hizo ilikuwa kero kwani watu hao, walipojibiwa kwamba Maalim Seif hajafariki dunia, hawakuamini.
Mwenyekiti wa CUF Taifa Profesa Ibrahim Lipumba alisema alipokea simu 50 kutoka Tanzania, Ulaya na Arabuni na baadaye kuamua kutoa sauti ya simu yake, ili kupata muda wa kufanya kazi zake.
"Nilistaajabu sana mana sijui ni nani aliyeanzisha uvumi ule, mimi mwenyewe nilipokea simu 50, nikaona kila muda ukienda simu zinazidi kuingia nikaamua kutoa sauti ya simu na kuendelea na kazi zangu.
"Kitu kimoja tu ambacho kilinifariji sana, ni kwa namna gani watanzania wa ndani na nje ya nchi wanavyompenda maalim Seif, maana ule mstuko haukuwa wa kawaida, hata hali ya nchi ilianza kubadilika hafla," alisema Profesa Lipumba.
Kwa upande wake Mkurugenzi Habari na Mahusiano na Umma wa CUF Salim Bimani alisema alipokea simu 1,685 na ujumbe mfupi wa simu ambao haukuwa na idadi kutoka kwa watu mbalimbali duniani.
"Kwa kweli nilipokea simu katika simu zangu zote mbili hadi masikio na kichwa kikaanza kuuma, lakini sikuweza kuzima simu wala kuzikwepa simu hizo, kwa sababu ingekuwa hatari zaidi. Nilipokea simu kutoka ndani na nje ya nchi, kutoka Uingereza na Arabuni," alisema Bimani.
Naye Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF Ashura Mustapha alisema alipokea simu 800 kutoka kwa watu mbalimbali, wakiwamo wananchi wa kawaida na waandishi wa habari wakitaka kufahamu ukweli wa mambo.
Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar Juma Duni Haji alisema alipokea simu 100 na baada ya hapo aliamua kuzima simu, kwa kuwa hakukua na umeme visiwani humo.
Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Hamad Rashid Mohammed alisema alipokea simu 256, na 12 kati hizo zilitoka kwa watu wa nchi za falme za kiarabu.
"Nilipokea simu nyingi kutoka Ujerumani, Kanada, Arabuni, Uingereza na Tanzania, kwa kweli ulikuwa mtikisiko, Zanzibar ilizizima ghafla," alisema Rashid ambaye pia ni mbunge wa Wawi Pemba (CUF).
Msaidizi wa Karibu wa Maalim Seif, Jussa Ismail Jussa alisema alipokea zaidi ya simu 100 kutoka kona mbalimbali za dunia.
Kwa kweli uvumi ulienea kwa kasi ya ajabu. Mimi na Bimani tuliongoza kwa kupokea simu nyingi na jumbe fupi za maandishi, peke yangu nilipokea simu 1,000, alisema Jussa.
Jussa alisema maalim Seif bado yupo katika hospitali ya Hindu Mandal akiendelea na matibabu na kwamba hali yake inaendelea kuwa nzuri.
CHANZO MWANANCHI
| Comments |
|
3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."
Habari Motomoto
-
Wahariri kujadili jinsi ya kuwasaidia wapiga kura wakati wa kampeni Wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini watakutana jijini...
-
Slaa apata mapokezi makubwa Musoma, Mwanza Maelfu ya wananchi, wakiwamo watumishi wa serikali, wafanyabiashara...
-
Jaji Mkuu: Hatukushinikizwa hukumu ya mgombea binafsi Jaji Mkuu wa Tanzania, Augustine Ramadhan, amesema uamuzi wa Mahakama...
-
Ajali ya basi yaua abiria 16 Watu 16 wamefariki dunia na wengine 48 kujeruhiwa baada ya basi la...
-
Kura ya maoni Z`bar yamg`oa DC Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, amemfukuza kazi Mkuu wa Wilaya...
-
Takukuru sasa inatawala nchi Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imewakamata makada...
-
Karume awa mbogo Z`bar Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume, amevunja ukimya kwa kusema kuwa...
-
Umati wamlaki Slaa jijini Arusha Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod...
-
Jaji Eliamani Mbise afariki dunia Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Eliamani Mbise, amefariki dunia...
-
Tume ya uchaguzi yataka ushahidi wizi wa kura Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeomba kupewa taarifa za mianya ya wizi...
-
Waibuka washindi Viti Maalum CCM Wagombea kadha wameibuka na ushindi katika mchuano wa kura za uteuzi...
-
Waziri Sitta azungumzia sakata ya Takukuru Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Magreth Sitta, amekanusha...
-
Kamanda Takukuru ashushwa cheo WAKATI habari za rushwa zikiendelea kutawala harakati za kuwania ...
- 1
- 2
- 3
- 4
- 5
- 6
- 7
- 8
- 9
- 10
- 11
- 12
- 13
- 14
- 15
- 16
- 17
- 18
- 19
- 20
Zilizosomwa Sana
- Schorlaships
- MAJINA YA WANAFUNZI 33658 WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO, VYUO VYA UFUNDI NA CHUO CHA MAJI MWAKA 2010
- United States
- CHAKULA CHA USIKU: WAHANGA SASA NI WANAWAKE! - Mwambie, usione haya
- AFYA! AFYA! Mambo yote muhimu haya hapa
- Dawa za Kuongeza Ufanisi wa Mwanaume Kitandani Zazinduliwa
- Europe
- Advertisement Plan
- ***BREAKING NEWS: Watuhumiwa wote kesi ya ZOMBE waachiliwa huru!!!***
- Aliyefumwa akibaka bintiye ala kichapo
- Australia
- Man Utd ushindi sasa basi
- Wanafunzi walioteketea kuzikwa kaburi moja leo
- Chanjo ya HIV yapunguza maambukizi
- United Kingdom
- Henry Joseph Shindika aula

