Saturday, July 31, 2010
   
Text Size

Tafuta kwenye Website hii

Marekani yaonya wingi wa bidhaa feki nchini

BALOZI wa Marekani nchini , Alfonso Lenhardt amesema biashara ya bidhaa na dawa feki iliyoshamiri katika nchi za Afrika Mashariki ni hatari kwa uchumi wa nchi hizo pamoja na afya za wananchi wake.

Balozi huyo aliyasema hayo jana wakati akifungua warsha ya siku mbili ya kutoa mafunzo juu ya namna ya kupambana na bidhaa feki kwa maofisa wa taasisi mbalimbali kutoka nchi wanachama wa jumuiya hiyo wanaohusika na kupamba na bidhaa hizo.

Kwa mujibu wa balozi huyu, biashara hizi mbali na kuhatarisha afya za watumiaji, pia zinasababisha nchi kukosa mapato ambayo yangetokana na kodi na pia wananchi kukosa kazi.

Katika hatua nyingine, Naibu Mkurugenzi wa Tume ya ushindani nchini Gregory Ndanu alisema katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, tume hiyo iliteketeza bidhaa feki zenye thamani ya Sh2 bilioni.

"Hawa wafanyabiashara wa bidhaa bandia wao wanachojali ni faida tu, mambo ya afya ya mtumiaji hawajui, kuteketeza hizi bidhaa inasaidia sana kwa sababu wengine hata wameshafilisika kutokana na bidhaa zao kuteketezwa," alisema Ndanu.

Ndanu ambaye pia alikuwa mshiriki katika semina hiyo iliyoandaliwa na Ubalozi wa Marekani nchini alisema ili kuimaliza biashara hiyo, lazima kuwe na bunge imara, mahakama imara, polisi wanaofuata sheria pamoja na maofisa wa forodha wanaofuata sheria katika ukaguzi.

"Hali ilivyo hivi sasa siyo imara, kuna matatizo katika ukaguzi wa bidhaa pamoja na ucheleweshwaji wa kesi katika mahakama zetu," alisema Ndanu.

Hata hivyo alisema katika Jumuiya ya Afrika Mashariki Tanzania inaongoza na kupambana na tatizo hilo kwa kulinganisha na nchi nyingine wanachama wa jumuiya hiyo.

CHANZO MWANANCHI

Comments
Add New Search
Write comment
Name:
Email:
 
Title:
UBBCode:
[b] [i] [u] [url] [quote] [code] [img] 
 
 
Please input the anti-spam code that you can read in the image.

3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."

Habari Motomoto

  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20

Login Form