Saturday, July 31, 2010
   
Text Size

Tafuta kwenye Website hii

Polisi yavunja maandamano Togo

Polisi wa kupambana na ghasia nchini Togo wamelazimika kutumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji zaidi ya 1,000 waliokuwa wamekusanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo, Lome, kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais.

Waandamanaji wenye hasira waliwapiga mawe na kuwatusi maafisa wa polisi waliokuwa wamejihami na silaha, huku wakipiga kelele na kutaka mageuzi na rais mpya.

Leo ni siku ya nne ya kuongezeka hali ya wasiwasi tangu Faure Gnassingbe alipotangazwa mshindi wa uchaguzi huo, ambao chama kikuu cha upinzani cha UFC kinasema ulikumbwa na udanganyifu.

Maandamano ya leo yalikuwa yamepigwa marufuku na serikali, lakini mgombea wa chama cha upinzani, Jean-Pierre Fabre, ameapa kufanya maandamano kila siku kupinga ushindi wa rais Gnassingbe.

Comments
Add New Search
Write comment
Name:
Email:
 
Title:
UBBCode:
[b] [i] [u] [url] [quote] [code] [img] 
 
 
Please input the anti-spam code that you can read in the image.

3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."

Habari Motomoto

  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20

Login Form