Kura za Rais kutangazwa majimboni
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesema kuwa matokeo ya Rais yatatangazwa kwenye majimbo badala ya kusubiriwa kutangazwa na NEC.
Mkurugenzi wa NEC, Rajabu Kiravu, alisema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na wawakilishi wa watu wenye ulemavu kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba, mwaka huu.
Alisema kuwa lengo la kufanya hivyo ni kuondoa hofu kwa wananchi wanaosubiri kujua matokeo.
Kiravu alisema kuwa NEC imeanza maandalizi ya uchaguzi ujao kwa kujipanga kikamilifu ili kuwepo na uwazi na haki sawa kwa mujibu wa sheria.
Alisema kwa sasa NEC inaboresha Daftari la Kudumu la Wapigakura ili iweze kupanga vituo vya kupigia kura wakati wa uchaguzi mkuu.
Alisema kwa mwaka huu vituo vitaongezeka kufikia vituo 55,000 kutoka 47,000 vya mwaka 2005.
Mkurugenzi huyo alisema asasi za kiraia zikiwemo za walemavu zina wajibu wa pekee wa kuelimisha umma hususan masuala muhimu yanayohusu uchaguzi.
Kwa mujibu wa Kiravu, uelimishaji huo ni ule unaolenga kumpa uelewa mpiga kura kuhusiana na namna ya kupiga kura, thamani ya kupiga kura, umihimu wa kutunza kadi ya kupigia kura na kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura.
Alisema walemavu watapewa kipaumbele zaidi kwa kuwa ni watu kama watu wengine na wana haki za msingi na watapatiwa elimu kuhusu namna ya kushiriki katika uchaguzi huo.
Mkuu wa Mradi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP), Oscar Harnam, alisema kuwa wamejitolea kwa ajili ya kuwasaidia walemavu kwenye uchaguzi na kuwapatia mahitaji watakayoyahitaji wakati wa uchaguzi.
Alisema takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 8.2 ni watu wenye ulemavu ambao ni sawa na watu zaidi ya milioni 3 hivyo wanapaswa kushiriki.
| Comments |
|
3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."
Habari Motomoto
-
Wahariri kujadili jinsi ya kuwasaidia wapiga kura wakati wa kampeni Wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini watakutana jijini...
-
Slaa apata mapokezi makubwa Musoma, Mwanza Maelfu ya wananchi, wakiwamo watumishi wa serikali, wafanyabiashara...
-
Jaji Mkuu: Hatukushinikizwa hukumu ya mgombea binafsi Jaji Mkuu wa Tanzania, Augustine Ramadhan, amesema uamuzi wa Mahakama...
-
Ajali ya basi yaua abiria 16 Watu 16 wamefariki dunia na wengine 48 kujeruhiwa baada ya basi la...
-
Kura ya maoni Z`bar yamg`oa DC Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, amemfukuza kazi Mkuu wa Wilaya...
-
Takukuru sasa inatawala nchi Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imewakamata makada...
-
Karume awa mbogo Z`bar Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume, amevunja ukimya kwa kusema kuwa...
-
Umati wamlaki Slaa jijini Arusha Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod...
-
Jaji Eliamani Mbise afariki dunia Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Eliamani Mbise, amefariki dunia...
-
Tume ya uchaguzi yataka ushahidi wizi wa kura Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeomba kupewa taarifa za mianya ya wizi...
-
Waibuka washindi Viti Maalum CCM Wagombea kadha wameibuka na ushindi katika mchuano wa kura za uteuzi...
-
Waziri Sitta azungumzia sakata ya Takukuru Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Magreth Sitta, amekanusha...
-
Kamanda Takukuru ashushwa cheo WAKATI habari za rushwa zikiendelea kutawala harakati za kuwania ...
- 1
- 2
- 3
- 4
- 5
- 6
- 7
- 8
- 9
- 10
- 11
- 12
- 13
- 14
- 15
- 16
- 17
- 18
- 19
- 20
Zilizosomwa Sana
- Schorlaships
- MAJINA YA WANAFUNZI 33658 WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO, VYUO VYA UFUNDI NA CHUO CHA MAJI MWAKA 2010
- United States
- CHAKULA CHA USIKU: WAHANGA SASA NI WANAWAKE! - Mwambie, usione haya
- AFYA! AFYA! Mambo yote muhimu haya hapa
- Dawa za Kuongeza Ufanisi wa Mwanaume Kitandani Zazinduliwa
- Europe
- Advertisement Plan
- ***BREAKING NEWS: Watuhumiwa wote kesi ya ZOMBE waachiliwa huru!!!***
- Aliyefumwa akibaka bintiye ala kichapo
- Australia
- Man Utd ushindi sasa basi
- Wanafunzi walioteketea kuzikwa kaburi moja leo
- Chanjo ya HIV yapunguza maambukizi
- United Kingdom
- Henry Joseph Shindika aula

