Saturday, July 31, 2010
   
Text Size

Tafuta kwenye Website hii

Mhandisi apata wakati mgumu mbele ya JK

Mhandisi wa Maji mkoani hapa, Mkama Bwire, juzi alipata wakati mgumu baada ya wananchi kumzomea mbele ya Rais Jakaya kikwete.

Bwire alifikwa na zahama hilo baada ya Rais kumuita mbele na kumuuliza kwa nini mkoa wa Tabora unakabiliwa na tatizo la maji.

Baada ya kusimama meza kuu, alianza kutoa maelezo lakini wananchi waliibuka na kuanza kumzomea kwa madai kuwa alichokuwa akimweleza Rais Kikwete ni uongo.

Wananchi hao walikuwa wamekusanyika kwenye uwanja wa Ali Hassani Mwinyi katika kilele cha Siku ya Wanawake Duniani.

Bwire baada ya kuzomewa alirudi tena jukwaani na kutoa maelezo ya ziada.

Baada ya maelezo ya mara ya pili, Rais Kikwete alianza kucheka na kumsifu kuwa ni mjanja wa kujieleza.

Alimwambia Kikwete kuwa tatizo la maji linatokana na uchakavu wa miundombinu ya mabomba na ongezeko la idadi ya watu.

Alimwambia Rais kuwa wanaendelea na mchakato wa kutafuta ufumbuzi wa tatizo la maji.

Kutokana na hali hiyo Rais Kikwete aliahidi kuangalia uwezekano wa kupeleka maji katika mkoa huo kutoka mkoani Shinyanga.

Alisema jambo hilo linawezekana na kwamba maji yanayotoka Shinyanga yanaweza kuwa suluhisho la kudumu.

Maji hayo yanatoka ziwa Victoria mkoani Mwanza ambapo alisema yatavutwa mpaka wilaya ya Nzega na kisha kuingiza Tabora mjini.

 

CHANZO: NIPASHE
Comments
Add New Search
Write comment
Name:
Email:
 
Title:
UBBCode:
[b] [i] [u] [url] [quote] [code] [img] 
 
 
Please input the anti-spam code that you can read in the image.

3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."

Habari Motomoto

  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20

Login Form