Watu 600 hawana makazi Mwanza
Familia zaidi ya 120 zenye takribani watu 600 hazina makazi kutokana madhara ya mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha usiku wa kuamkia juzi mkoani Mwanza.
Watu hao wakitaabika, majina ya watu wanne kati ya watano waliofariki kutokana na mafuriko yaliyosabaishwa na mvua hizo yametajwa.
Waliofariki wametajwa kuwa ni Martha Samwel (25) na Yunis Peter (25) ambao ni wakazi wa Kisesa wilayani Magu, Wankuru Kilali (65) mkazi wa Kiseke na Mashauri Masasila (60), mkazi wa Buswelu jijini hapa. Mmoja bado hajafahamika.
Mkazi mwingine, Philemon William (25) alijeruhiwa na kulazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mwanza ya Sekou Toure baada ya kuangukiwa na nyumba.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Nonosius Komba, alisema waathirika wa maafa hayo wamehifadhiwa katika shule za sekondari, msingi na kwenye maghala.
Akifafanua kufuatia mvua hiyo iliyoleta maafa makubwa, Kamanda Komba alisema katika eneo la Kisesa wilayani Magu nyumba 21 zilibomoka, wakati katika kijiji cha Ihushi nyumba 119 zilibomoka.
Alitaja vijiji vilivyoathirika na idadi ya nyumba zilizobomka kwenye mabano kuwa ni Sese (30), Matale (36), Buswelu (2) na Kiseke (1).
Komba alisema kufuatia maafa hayo, tathmini itaendelea kufanyika kubaini ukubwa wa tatizo pamoja na madhara yaliyopatikana kutokana na mvua hiyo na kwamba taarifa zaidi zitatolewa.
Kamanda Komba alisema marehemu wote waliangukiwa na kuta za nyumba wanazoishi wakati mafuriko hayo yalipotokea.
Wakati huo huo serikali ya Mkoa wa Mwanza imeanza kuwasaidia watu walioathirika na mafuriko ambao wapo kwenye majengo ya shule kwa kuwahudumia kwa chakula na kuwatafutia maturubai kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za muda.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Abbas Kandoro, alisema watu hao kwa sasa wamehifadhiwa katika Shule ya Sekondari ya Ihushi kwenye jengo la utawala pamoja na nyumba ya mwalimu, lengo likiwa ni kutoathiri wanafunzi wanaoendelea na masomo.
Kandoro alisema kuwa barabara iliyokuwa imefungwa ya kuelekea Igombe kutokana na daraja lake kukatika kutokana na mafuriko hayo, imefunguliwa na mabasi yameruhusiwa kuanza kupita.
Kwa mujibu wa Kandoro, hatua hiyo imewezesha huduma ya usafiri kurejea katika hali ya kawaida wakati ukarabati ukiendelea.
Aidha, Kandoro amewataka wakazi wa mabondeni kuachana na ubishi na kukubali maelekezo yanayotolewa na viongozi.
“Unajua ndio natoka huko sasa hivi, kama kijiji cha Ihushi walioathirika wengi ni wakazi wa mabondeni na walikwishaelezwa muda mrefu kuwa wahame kutokana na kuwepo kwa tishio la mvua za El-nino, lakini waliendelea kukaidi maelezo ya viongozi,” alisema Kandoro.
| Comments |
|
3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."
Habari Motomoto
-
JK aahidi kuanzisha programu ya malisho Mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete,...
-
Kesi ya Mramba ya nguruma Kesi ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia hasara serikali...
-
Maelfu wajitokeza kumuaga Kalumuna Wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakiwemo watu wenye ulemavu jana...
-
CCM yazuia wagombea kushiriki midahalo TBC CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimewazuia wagombea wake wa ubunge kushiriki...
-
Mchungaji amfyeka vidole mtoto kanisani MTOTO wa kike aliyetajwa kwa jina la Anna Danken (17) wa Kijiji ...
-
ZEC yaanza kusilikiza pingamizi mgombea CUF Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), imeanza kusikiliza rufaa ya mgombea...
-
JK: Vyama vya upinzani vya msimu MGOMBEA urais kupitia CCM, Jakaya Kikwete ameviponda vyama vya upinzani...
-
Profesa Baregu avamiwa garini Mwenyekiti wa kamati ya kampeni ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo...
-
Mikoa 14 kukumbwa na ukame Baa la njaa linainyemelea Tanzania kutokana na utabiri wa hali ya...
-
Gari la mkuu wa kampeni Chadema lavunjwa vioo MWENYEKITI wa Kamati ya Kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo...
-
Walimu mbaroni wizi wa mitihani ya darasa la sab WALIMU wakuu na wasimamizi wa mitihani, wanashikiliwa na polisi na...
-
Mahakama: Chenge ana kesi ya kujibu Mahakama ya wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam imesema mgombea...
-
Vyama 15 vyasaini rasimu ya mwongozo wa maadili Z`bar Viongozi wa vyama 15 vya siasa jana walisaini rasimu ya mwongozo...
- 1
- 2
- 3
- 4
- 5
- 6
- 7
- 8
- 9
- 10
- 11
- 12
- 13
- 14
- 15
- 16
- 17
- 18
- 19
- 20
Zilizosomwa Sana
- Schorlaships
- MAJINA YA WANAFUNZI 33658 WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO, VYUO VYA UFUNDI NA CHUO CHA MAJI MWAKA 2010
- United States
- CHAKULA CHA USIKU: WAHANGA SASA NI WANAWAKE! - Mwambie, usione haya
- Dawa za Kuongeza Ufanisi wa Mwanaume Kitandani Zazinduliwa
- AFYA! AFYA! Mambo yote muhimu haya hapa
- Europe
- ***BREAKING NEWS: Watuhumiwa wote kesi ya ZOMBE waachiliwa huru!!!***
- Advertisement Plan
- Australia
- Aliyefumwa akibaka bintiye ala kichapo
- Man Utd ushindi sasa basi
- Ratiba ya Ligi Kuu Uingereza 2010/2011
- Chanjo ya HIV yapunguza maambukizi
- Wanafunzi walioteketea kuzikwa kaburi moja leo
- Japan

