Watu 600 hawana makazi Mwanza
Familia zaidi ya 120 zenye takribani watu 600 hazina makazi kutokana madhara ya mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha usiku wa kuamkia juzi mkoani Mwanza.
Watu hao wakitaabika, majina ya watu wanne kati ya watano waliofariki kutokana na mafuriko yaliyosabaishwa na mvua hizo yametajwa.
Waliofariki wametajwa kuwa ni Martha Samwel (25) na Yunis Peter (25) ambao ni wakazi wa Kisesa wilayani Magu, Wankuru Kilali (65) mkazi wa Kiseke na Mashauri Masasila (60), mkazi wa Buswelu jijini hapa. Mmoja bado hajafahamika.
Mkazi mwingine, Philemon William (25) alijeruhiwa na kulazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mwanza ya Sekou Toure baada ya kuangukiwa na nyumba.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Nonosius Komba, alisema waathirika wa maafa hayo wamehifadhiwa katika shule za sekondari, msingi na kwenye maghala.
Akifafanua kufuatia mvua hiyo iliyoleta maafa makubwa, Kamanda Komba alisema katika eneo la Kisesa wilayani Magu nyumba 21 zilibomoka, wakati katika kijiji cha Ihushi nyumba 119 zilibomoka.
Alitaja vijiji vilivyoathirika na idadi ya nyumba zilizobomka kwenye mabano kuwa ni Sese (30), Matale (36), Buswelu (2) na Kiseke (1).
Komba alisema kufuatia maafa hayo, tathmini itaendelea kufanyika kubaini ukubwa wa tatizo pamoja na madhara yaliyopatikana kutokana na mvua hiyo na kwamba taarifa zaidi zitatolewa.
Kamanda Komba alisema marehemu wote waliangukiwa na kuta za nyumba wanazoishi wakati mafuriko hayo yalipotokea.
Wakati huo huo serikali ya Mkoa wa Mwanza imeanza kuwasaidia watu walioathirika na mafuriko ambao wapo kwenye majengo ya shule kwa kuwahudumia kwa chakula na kuwatafutia maturubai kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za muda.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Abbas Kandoro, alisema watu hao kwa sasa wamehifadhiwa katika Shule ya Sekondari ya Ihushi kwenye jengo la utawala pamoja na nyumba ya mwalimu, lengo likiwa ni kutoathiri wanafunzi wanaoendelea na masomo.
Kandoro alisema kuwa barabara iliyokuwa imefungwa ya kuelekea Igombe kutokana na daraja lake kukatika kutokana na mafuriko hayo, imefunguliwa na mabasi yameruhusiwa kuanza kupita.
Kwa mujibu wa Kandoro, hatua hiyo imewezesha huduma ya usafiri kurejea katika hali ya kawaida wakati ukarabati ukiendelea.
Aidha, Kandoro amewataka wakazi wa mabondeni kuachana na ubishi na kukubali maelekezo yanayotolewa na viongozi.
“Unajua ndio natoka huko sasa hivi, kama kijiji cha Ihushi walioathirika wengi ni wakazi wa mabondeni na walikwishaelezwa muda mrefu kuwa wahame kutokana na kuwepo kwa tishio la mvua za El-nino, lakini waliendelea kukaidi maelezo ya viongozi,” alisema Kandoro.
| Comments |
|
3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."
Habari Motomoto
-
Wahariri kujadili jinsi ya kuwasaidia wapiga kura wakati wa kampeni Wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini watakutana jijini...
-
Slaa apata mapokezi makubwa Musoma, Mwanza Maelfu ya wananchi, wakiwamo watumishi wa serikali, wafanyabiashara...
-
Jaji Mkuu: Hatukushinikizwa hukumu ya mgombea binafsi Jaji Mkuu wa Tanzania, Augustine Ramadhan, amesema uamuzi wa Mahakama...
-
Ajali ya basi yaua abiria 16 Watu 16 wamefariki dunia na wengine 48 kujeruhiwa baada ya basi la...
-
Kura ya maoni Z`bar yamg`oa DC Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, amemfukuza kazi Mkuu wa Wilaya...
-
Takukuru sasa inatawala nchi Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imewakamata makada...
-
Karume awa mbogo Z`bar Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume, amevunja ukimya kwa kusema kuwa...
-
Umati wamlaki Slaa jijini Arusha Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod...
-
Jaji Eliamani Mbise afariki dunia Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Eliamani Mbise, amefariki dunia...
-
Tume ya uchaguzi yataka ushahidi wizi wa kura Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeomba kupewa taarifa za mianya ya wizi...
-
Waibuka washindi Viti Maalum CCM Wagombea kadha wameibuka na ushindi katika mchuano wa kura za uteuzi...
-
Waziri Sitta azungumzia sakata ya Takukuru Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Magreth Sitta, amekanusha...
-
Kamanda Takukuru ashushwa cheo WAKATI habari za rushwa zikiendelea kutawala harakati za kuwania ...
- 1
- 2
- 3
- 4
- 5
- 6
- 7
- 8
- 9
- 10
- 11
- 12
- 13
- 14
- 15
- 16
- 17
- 18
- 19
- 20
Zilizosomwa Sana
- Schorlaships
- MAJINA YA WANAFUNZI 33658 WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO, VYUO VYA UFUNDI NA CHUO CHA MAJI MWAKA 2010
- United States
- CHAKULA CHA USIKU: WAHANGA SASA NI WANAWAKE! - Mwambie, usione haya
- AFYA! AFYA! Mambo yote muhimu haya hapa
- Dawa za Kuongeza Ufanisi wa Mwanaume Kitandani Zazinduliwa
- Europe
- Advertisement Plan
- ***BREAKING NEWS: Watuhumiwa wote kesi ya ZOMBE waachiliwa huru!!!***
- Aliyefumwa akibaka bintiye ala kichapo
- Australia
- Man Utd ushindi sasa basi
- Wanafunzi walioteketea kuzikwa kaburi moja leo
- Chanjo ya HIV yapunguza maambukizi
- United Kingdom
- Henry Joseph Shindika aula

