Saturday, July 31, 2010
   
Text Size

Tafuta kwenye Website hii

Papandreou kukutana na Obama leo

Waziri mkuu wa Ugiriki, George Papandreou, anatarajiwa kukutana na rais wa Marekani Barack Obama mjini Washington hii leo. Mkutano kati ya viongozi hao unafanyika wakati kukiwa na wasiwasi kwamba walanguzi wa fedha wanahujumu juhudi za Ugiriki

kuondokana na tatizo kubwa la deni. Papandreou amesema ana matumaini ya kumshawishi rais Obama kwamba Marekani haiwezi kulipuuzilia mbali tatizo la kifedha linaloikabili Ugiriki.

 

Katika hotuba yake ya kwanza wakati alipowasili mjini Washington hapo jana, waziri Papandreou ameonya kwamba athari zitakazotokana na njama ya kuisambaratisha sarafu ya euro zitaiathiri pia Marekani na ametaka Ulaya na Marekani zishirikiane kupambana na walanguzi.

George Papandreou anatarajiwa pia kukutana na waziri wa fedha wa Marekani, Timothy Geithner, kujadiliana kuhusu mzozo wa fedha wa Ugiriki.

Comments
Add New Search
Write comment
Name:
Email:
 
Title:
UBBCode:
[b] [i] [u] [url] [quote] [code] [img] 
 
 
Please input the anti-spam code that you can read in the image.

3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."

Habari Motomoto

  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20

Login Form