Ndege ya ATCL yapata hitilafu angani
Ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), juzi ilikwamisha safari ya maofisa kadhaa waandamizi wa serikali waliokuwa wakienda mkoani Tabora kuhudhuria kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
Ndege hiyo iliondoka jijini Dar es Salaam juzi ikiwa imewachukua maofisa hao wa serikali, lakini ililazimika kurudi njiani baada ya kupata matatizo ya kiufundi wakati ikiwa angani.
Baadhi ya maofisa hao wa serikali (majina tunayo) waliozungumza na Nipashe jana, walithibitisha ndege hiyo kupatwa na hitilafu wakati ikiwa angani na hivyo, kulazimika kukatisha safari na kurejea jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa ATC, William Haji, alipoulizwa jana na Nipashe alisema tatizo lililoisibu ndege hiyo halikuwa kubwa kama linavyokuzwa.
“Kama kungekuwapo na hitilafu ningejua, lakini kama lilikuwapo, ni mambo ya kurekebishika tu,” alisema Haji.
Alisema kilichotokea kwa ndege hiyo, ni kuchelewa muda wa kwenda mkoani Kigoma, ambao mwisho wake ni saa 9:00 alasiri, jambo ambalo lililazimisha safari hiyo kusitishwa kwa vile kuna tatizo la taa za uwanjani.
Hata hivyo, alisema siku hiyo hiyo, ndege hiyo ilikwenda mkoani Mwanza, kwa kuwa uwanja wake una taa na jana ilikwenda Kigoma na kuongeza kuwa mzigo wa gharama za kuwahifadhi abiria waliokwama kusafiri, ulibebwa na shirika.
Maadhimisho hayo, ambayo kilele chake kilihitimishwa katika uwanja wa mpira wa Ali Hassan Mwinyi, mkoani humo, yaliyohutubiwa na Rais Jakaya Kikwete.
| Comments |
|
3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."
Habari Motomoto
-
Wahariri kujadili jinsi ya kuwasaidia wapiga kura wakati wa kampeni Wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini watakutana jijini...
-
Slaa apata mapokezi makubwa Musoma, Mwanza Maelfu ya wananchi, wakiwamo watumishi wa serikali, wafanyabiashara...
-
Jaji Mkuu: Hatukushinikizwa hukumu ya mgombea binafsi Jaji Mkuu wa Tanzania, Augustine Ramadhan, amesema uamuzi wa Mahakama...
-
Ajali ya basi yaua abiria 16 Watu 16 wamefariki dunia na wengine 48 kujeruhiwa baada ya basi la...
-
Kura ya maoni Z`bar yamg`oa DC Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, amemfukuza kazi Mkuu wa Wilaya...
-
Takukuru sasa inatawala nchi Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imewakamata makada...
-
Karume awa mbogo Z`bar Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume, amevunja ukimya kwa kusema kuwa...
-
Umati wamlaki Slaa jijini Arusha Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod...
-
Jaji Eliamani Mbise afariki dunia Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Eliamani Mbise, amefariki dunia...
-
Tume ya uchaguzi yataka ushahidi wizi wa kura Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeomba kupewa taarifa za mianya ya wizi...
-
Waibuka washindi Viti Maalum CCM Wagombea kadha wameibuka na ushindi katika mchuano wa kura za uteuzi...
-
Waziri Sitta azungumzia sakata ya Takukuru Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Magreth Sitta, amekanusha...
-
Kamanda Takukuru ashushwa cheo WAKATI habari za rushwa zikiendelea kutawala harakati za kuwania ...
- 1
- 2
- 3
- 4
- 5
- 6
- 7
- 8
- 9
- 10
- 11
- 12
- 13
- 14
- 15
- 16
- 17
- 18
- 19
- 20
Zilizosomwa Sana
- Schorlaships
- MAJINA YA WANAFUNZI 33658 WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO, VYUO VYA UFUNDI NA CHUO CHA MAJI MWAKA 2010
- United States
- CHAKULA CHA USIKU: WAHANGA SASA NI WANAWAKE! - Mwambie, usione haya
- AFYA! AFYA! Mambo yote muhimu haya hapa
- Dawa za Kuongeza Ufanisi wa Mwanaume Kitandani Zazinduliwa
- Europe
- Advertisement Plan
- ***BREAKING NEWS: Watuhumiwa wote kesi ya ZOMBE waachiliwa huru!!!***
- Aliyefumwa akibaka bintiye ala kichapo
- Australia
- Man Utd ushindi sasa basi
- Wanafunzi walioteketea kuzikwa kaburi moja leo
- Chanjo ya HIV yapunguza maambukizi
- United Kingdom
- Henry Joseph Shindika aula

