Saturday, July 31, 2010
   
Text Size

Tafuta kwenye Website hii

Mvua yaleta madhara, yabomoa nyumba 175 Mwanza

NYUMBA 175 zimeanguka kutokana na mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali kunyesha usiku wa kuamkia juzi na kusababisha vifo vya watu wanne akiwemo mtoto wa umri wa miaka sita huku familia 86 zikikosa makazi.

Nyumba hizo zilibomolewa na mvua hiyo katika Kijiji cha Kisesa, Kijiji cha Matale, Kijiji cha Ihishi, na Kiseke na kwamba nyumba 21 zilianguka Kisesa kilicho wilayani Magu na kusababisha vifo vya watu wawili na kujeruhi mmoja.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, kaimu kamanda wa polisi wa mkoa, Monosius Komba aliwataja watu waliofariki katika kijiji hicho kuwa ni Marthar Samweli, 25, na Yunus Peter, 25, wakati Freeman alijeruhiwa na kulazwa Hospitali ya Sekou Toure.

Komba alisema kuwa katika Kijiji cha Ihishi, nyumba 119 zilizokuwa zimejengwa kwa matofali ya tope zilianguka usiku huo na kusababisha familia 86 kukosa makazi na mtu mmoja kujeruhiwa.

Komba alimtaja majeruhi aliyeangukiwa na nyumba kuwa ni Sophia Changaa, 26, ambaye hali yake inaendelea vizuri baada ya kupata matibabu.

Alisema kuwa vijiji vingine ambavyo vilipata madhara ya mvua hiyo na kusababisha nyumba kuanguka ni pamoja na Kisesa kilicho wilayani Ilemela ambako nyumba 30 zilinguka lakini hakukuwa na madhara, wakati nyumba tatu zilianguka katika Kijiji cha Matale kilicho Kata ya Sangabuye.

Komba alisema kuwa katika kijiji cha Kiseke B wilayani Ilemela, nyumba moja ya Charles Kishorogo, 45, ilianguka majira ya saa 10:00 usiku na kusababisha kifo cha mtoto mmoja aliyetambulika kwa jina la Wankumu Kirari, 6, wakati katika wilaya mpya ya Busweru mtu moja aliyetambulika kwa jina la Mashauri Masasira, 60, aliangukiwa na nyumba yake na kufariki papo hapo.

Kamanda Komba alisema kuwa tathmini ya athari za maafa bado inafanyiwa kazi na taarifa za maafa hayo zitatolewa baadaye na kwamba watu waliobomokewa na nyumba zao wamepewa hifadhi katika shule za sekondari na msingi.

Mjini Mwanza, mvua hizo zilisababisha maji kujaa kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwanza kutokana na mkondo wa Mto Kimilabagalu ambao ulifurika maji yaliyotoka maeneo ya karibu na mto huo.

Akizungumza na waandishi wa habari kaimu meneja ,Mchunguzi Byantao alisema mvua hiyo ilinyesha muda mfupi na kusababisha uwanja huo kujaa maji.

Kaimu meneja wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Daniel Njenga aliwaambia waandishi wa habari kuwa kujaa kwa uwanja huo kunatokana na mkono wa mto huo kupitia hapo na kushindwa kudhibitiwa ili usiweze kuingiza maji uwanjani.

Alisema kila mvua zinaponyesha na maji kutoka mto huo yamekuwa yakiingia na kujaa katika eneo la uwanja na hivyo kuufanya kuwa katika mazingira ambayo si mazuri kwa ndege kutua na hivyo kuiomba serikali kuangalia uwezekano wa kudhibiti mto huo.

Mvua hizo zilianza kunyesha Machi 7 na kusababisha athari kubwa ikiwemo kujaa maji na kusabaisha uwanja huo kufungwa kwa muda juzi.

CHANZO MWANANCHI

Comments
Add New Search
Write comment
Name:
Email:
 
Title:
UBBCode:
[b] [i] [u] [url] [quote] [code] [img] 
 
 
Please input the anti-spam code that you can read in the image.

3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."

Habari Motomoto

  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20

Login Form