Saturday, July 31, 2010
   
Text Size

Tafuta kwenye Website hii

Marekani yaitaka Nigeria ichunguze mauaji

Marekani na mashirika ya kutetea haki za binadamu yameitaka Nigeria iyachunguze kwa uangalifu mauaji ya watu takriban 400 waliouwawa wakati wafugaji Waislamu walipovivamia vijiji vya Wakristo karibu na mji wa Jos,

nchini Nigeria.

Nigeria pia imetakiwa kuwafungulia mashtaka watu waliohusika na mauaji ya watu hao ambao wamezikwa kwenye kaburi la pamoja. Maafisa wa usalama wa Nigeria wanasema wamewatia mbaroni washukiwa 95 wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji hayo.

Kamishna mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na haki za binadamu, Navi Pillay, amesema amesikitishwa na mauaji hayo. Akizungumza mjini Geneva, Uswis,i hii leo Pillay amesisitiza kwamba juhudi za kupambana na umwagaji damu nchini humo hazitakiwi kuzingatia hatua za kiusalama pekee, na ameitolea wito Nigeria itatue matatizo ya kimsingi yanayosababisha kuzuka mara kwa mara mauaji ya kikabila na kidini.

Comments
Add New Search
Write comment
Name:
Email:
 
Title:
UBBCode:
[b] [i] [u] [url] [quote] [code] [img] 
 
 
Please input the anti-spam code that you can read in the image.

3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."

Habari Motomoto

  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20

Login Form