Vigogo wa Rites waanza kutimka
WAKATI serikali ikitarajiwa kutoa tamko la mustakabali wa shirika mahututi la reli, TRL kesho, tayari mameneja wa kampuni ya Rites ya India inayoendesha shirika hilo wameanza kutimka kurejea kwao.
Rais Jakaya Kikwete alidokeza juzi wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kuwa hatma ya shirika hilo muhimu na kongwe nchini itajulikana kesho baada ya kufanyika kwa mazungumzo, lakini hakufafanua kauli yake.
Lakini Mwananchi imedokezwa kuwa vigogo watatu wa TRL wameshatimka na kurejea kwao India hata kabla ya kutangazwa kwa uamuzi wa mwisho juu ya shirika hilo lililokuwa likiendesha huduma ya usafiri wa reli kati ya Dar es salaam na mikoa ya Kati na Kanda ya Ziwa.
Vyanzo vya uhakika vya habari vilithibitishia gazeti hili kuondoka kwa mameneja hao ambao uongozi wao umekumbwa na kikwazo kikubwa kutoka kwa wafanyakazi wa shirika hilo ambao wamekuwa wakiendesha migomo mara kwa mara.
Hata hivyo, Naibu Waziri wa Miundombinu Hezekiah Chibulunje hakutaka kuthibitisha au kukanusha taarifa za kuondoka kwa vigogo hao na badala yake akawataka wananchi kusubiri ahadi ya rais kesho.
"Mheshimiwa rais ameshasema; mimi nikisema kitu hapa itakuwa ni utovu wa nidhamu. Tusubiri ahadi ya rais aliyotoa kwamba kila kitu kitajulikana Alhamisi," alifafanua Chibulunje.
Alipoulizwa maendeleo ya mchakato wa serikali kununua hisa asilimia 51 za Rites, alijibu: "Nafikiri haitakuwa sahihi Rais kazungumza jana mimi nizungumze leo, subiri alhamisi ikipita njoo."
Mpashaji wa habari hizo aliiambia Mwananchi akisema: "Mameneja watatu wameondoka kurejea India; wamechoka na mambo yalivyo sasa... serikali inahaha kununua hisa lakini majadiliano ya bei bado yanaendeleo."
Kwa mujibu wa chanzo hicho, kikao cha Baraza la Mawaziri ndicho kinasubiriwa kupata mwafaka wa pamoja kuhusu hatua ambayo inapaswa kupigwa na serikali katika kipindi hiki.
Mkataba kati ya Rites, inayomiliki asilimia 51 ya hisa za TRL, na serikali yenye hisa asilimia 49, ulisainiwa Oktoba 2007 na ni wa miaka 25, lakini umekuwa ukikumbwa na matatizo kadhaa ya kiuendeshaji.
CHANZO MWANANCHI
| Comments |
|
3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."
Habari Motomoto
-
Wahariri kujadili jinsi ya kuwasaidia wapiga kura wakati wa kampeni Wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini watakutana jijini...
-
Slaa apata mapokezi makubwa Musoma, Mwanza Maelfu ya wananchi, wakiwamo watumishi wa serikali, wafanyabiashara...
-
Jaji Mkuu: Hatukushinikizwa hukumu ya mgombea binafsi Jaji Mkuu wa Tanzania, Augustine Ramadhan, amesema uamuzi wa Mahakama...
-
Ajali ya basi yaua abiria 16 Watu 16 wamefariki dunia na wengine 48 kujeruhiwa baada ya basi la...
-
Kura ya maoni Z`bar yamg`oa DC Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, amemfukuza kazi Mkuu wa Wilaya...
-
Takukuru sasa inatawala nchi Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imewakamata makada...
-
Karume awa mbogo Z`bar Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume, amevunja ukimya kwa kusema kuwa...
-
Umati wamlaki Slaa jijini Arusha Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod...
-
Jaji Eliamani Mbise afariki dunia Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Eliamani Mbise, amefariki dunia...
-
Tume ya uchaguzi yataka ushahidi wizi wa kura Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeomba kupewa taarifa za mianya ya wizi...
-
Waibuka washindi Viti Maalum CCM Wagombea kadha wameibuka na ushindi katika mchuano wa kura za uteuzi...
-
Waziri Sitta azungumzia sakata ya Takukuru Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Magreth Sitta, amekanusha...
-
Kamanda Takukuru ashushwa cheo WAKATI habari za rushwa zikiendelea kutawala harakati za kuwania ...
- 1
- 2
- 3
- 4
- 5
- 6
- 7
- 8
- 9
- 10
- 11
- 12
- 13
- 14
- 15
- 16
- 17
- 18
- 19
- 20
Zilizosomwa Sana
- Schorlaships
- MAJINA YA WANAFUNZI 33658 WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO, VYUO VYA UFUNDI NA CHUO CHA MAJI MWAKA 2010
- United States
- CHAKULA CHA USIKU: WAHANGA SASA NI WANAWAKE! - Mwambie, usione haya
- AFYA! AFYA! Mambo yote muhimu haya hapa
- Dawa za Kuongeza Ufanisi wa Mwanaume Kitandani Zazinduliwa
- Europe
- Advertisement Plan
- ***BREAKING NEWS: Watuhumiwa wote kesi ya ZOMBE waachiliwa huru!!!***
- Aliyefumwa akibaka bintiye ala kichapo
- Australia
- Man Utd ushindi sasa basi
- Wanafunzi walioteketea kuzikwa kaburi moja leo
- Chanjo ya HIV yapunguza maambukizi
- United Kingdom
- Henry Joseph Shindika aula

