Saturday, July 31, 2010
   
Text Size

Tafuta kwenye Website hii

Mrema adai Spika Sitta amlipe Sh 1 bilioni

HATIMAYE mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP), Augustine Mrema ameanza rasmi mchakato wa kumfikisha mahakamani spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Samwel Sitta baada ya kumwandikia barua ya kumtaka amuombe radhi na kumlipa fidia ya Sh 1bilioni.

Mrema amefikia uamuzi huo siku mbili tu tangu atangaze kusudio la kumshtaki mahakamani kiongozi huyo wa Bunge ambaye alimuelezea Mrema kuwa ni mtu aliyefilisika kisiasa na kifedha na kufikia hatua ya kusema kuwa anapewa fedha na CCM ili aipigie debe.

Sitta alizungumza hayo baada ya Mrema kuitisha mkutano na waandishi wa habari na kumtuhumu spika huyo kuwa ana makundi kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano na kwamba anakiuka sheria na taratibu za Bunge kwa kuendelea kuzungumzia suala la kashfa ya Richmond nje ya chombo hicho cha kutunga sheria.

Lakini majibu ya Sitta yalimfanya Mrema angake na kuamua kuweka hadharani kiasi cha akiba ya fedha alichonacho kwenye akaunti yake ya benki na kutishia kuwa atampeleka spika huyo mahakamani iwapo atashindwa kutoa ushahidi wa tuhuma zake.

"Mheshimiwa Samwel Sitta Spika wa Bunge la Tanzania, nakuarifu rasmi kwamba nakusudia kukufungulia kesi ya madai kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania kutokana na kauli zako ulizozitoa magazetini dhidi yangu," anasema Mrema ambaye aliwahi kuwa mbunge wa jimbo la Vunjo kwa tiketi ya CCM na baadaye Temeke kwa tiketi ya NCCR Mageuzi.

Katika barua yake hiyo yenye kumbukumbu namba TLP/HQ/SIR/03/55 ya Machi 8 mwaka huu, Mrema amempa Spika Sitta siku saba amuombe radhi katika magazeti yaliyomnukuu kwa uzito ulele na kumlipa fidia hiyo katika muda huo.

Akizungumza na Mwananchi jana kwenye ofisi za makao makuu ya TLP yaliyo Magomeni akiwa ameshika barua hiyo, Mrema alisema: "Spika alikaririwa na magazeti akisema kuwa mimi Mrema ni mhuni, nimepitwa na wakati, pia nimefilisika kisiasa na kipesa... sasa ninatafuta njia ya kujinasua katika hali hiyo.

"Katika gazeti jingine alisema kuwa kuna uwezekano kuwa nimepata pesa ili niipigie debe CCM; gazeti jingine akasema kuwa Mrema ni muhu

Mrema, ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani alisema kuwa, kauli za Sitta zimemdhalilisha mbele ya jamii akiwa kama Mwenyekiti wa TLP hali iliyosababisha wanachama 500,000 wa chama hicho nchini wakose imani naye.

"Nikiwa mwenyekiti wa TLP, chama cha nne kwa ukubwa nchini, kauli za Sitta hazivumiliki amenikashifu na kunitukana, wanachama wa TLP wamekosa imani na mimi kutokana na kauli hizo, "alisema Mrema.

"Pia kauli zako zimenivunjia heshima niliyojijengea katika utumishi wangu uliotukuka serikalini ambako nilifanya kazi kwa zaidi ya miaka 30 nikiwa ofisa usalama wa taifa, mbunge, waziri na baadaye Naibuwa Waziri Mkuu."

Mrema alisema kuwa kauli hizo za Sitta zimemuathiri kwa kuwa ameshajitangaza kugombea ubunge katika jimbo la Vunjo kwa kuwa kauli hizo zinaweza kutumiwa na wapinzani wake kummaliza kisiasa.

CHANZO MWANANCHI

Comments
Add New Search
Write comment
Name:
Email:
 
Title:
UBBCode:
[b] [i] [u] [url] [quote] [code] [img] 
 
 
Please input the anti-spam code that you can read in the image.

3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."

Habari Motomoto

  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20

Login Form