Saturday, July 31, 2010
   
Text Size

Tafuta kwenye Website hii

Wanaougua fistula waomba msaada

Wanawake wanaougua ugonjwa wa Fistula, wameiomba serikali kuwawekea matibabu kila mkoa ili kuwasaidia kupata huduma kwa urahisi kwa kuwa inawagharimu kiasi kikubwa cha fedha kusafiri hadi jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, mmoja wa wagonjwa huo ambaye amelazwa katika Hospitali ya CCBRT, Paulina Chaula (34), Mkazi wa Mkoa wa Dodoma, alisema kumekuwepo na tatizo kubwa la ukosefu wa huduma hiyo katika mikoa mbalimbali nchini.

Alisema kuwa alipata ugonjwa huo alipojifungua mtoto wa nane na tatizo hilo lilimsumbua kwa mwaka mmoja na miezi mitatu.

Chaula alisema baada ya kuugua kwa muda mrefu, ndipo alipopatiwa taarifa kuwa huduma hiyo inatolewa katika CCBRT na ndipo alipoamua kuitafuta.

Aidha alisema fistula imekuwa ni ugonjwa ambao huwaletea madhara makubwa kwa wanawake ikiwemo kutokufanya kazi nzito, kuachwa na wanaume.

Aliiomba serikali kutoa msaada kwa wanawake ambao wameathirika na ugonjwa huo ili waweze kupatiwa matibabu.

Mratibu wa masuala ya Ufundi wa Uzazi katika Hospitali hiyo, Dk. Brenda D'emerlo, alisema katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani iliyoadhimishwa jana, madaktari wanawake walijitolea kutibu ugonjwa huo bure na hata kuwafariji baadhi wa wagonjwa.

Aidha, lisema kuwa ugonjwa huo unaweza kutoweka endapo tu kutakuwa na huduma bora katika suala zima la uzazi wa mpango ikiwemo na kumjali mama anapokuwa mjamzito.

Daktari wa magonjwa ya wanawake katika hospitali hiyo, Vindhya Pakirama, alisema ugonjwa huo hutibiwa kwa muda wa wiki mbili au mwezi.

 

CHANZO: NIPASHE
Comments
Add New Search
Write comment
Name:
Email:
 
Title:
UBBCode:
[b] [i] [u] [url] [quote] [code] [img] 
 
 
Please input the anti-spam code that you can read in the image.

3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."

Habari Motomoto

  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20

Login Form