Mke wa Balozi auawa kinyama na shamba boi
Mke wa Balozi mwandamizi mstaafu wa Tanzania nchini Marekani, Andrew Daraja, ameuawa kinyama kwa kuchomwa kisu cha kifuani sehemu ya titi la kushoto na polisi wanamtafuta mhudumu wa shamba, James Mabakuri (22), kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Elias Kalinga, alimtaja mke huyo wa balozi kuwa ni Anna Daraja, mkazi wa Kimara Temboni, jijini Dar es Salaam.
Kamanda Kalinga aliiambia Nipashe kuwa mauaji hayo yalitokea juzi nyumbani kwa Balozi Daraja Temboni, jijini Dar es Salaam wakati balozi akiwa safarini mkoani Tanga.
Kamanda Kalinga alisema kuwa mtuhumiwa huyo ambaye wanaendelea kumtafuta, mara baada ya tukio hilo anadaiwa kuiba kiasi ya Sh. milioni 2 na kutoweka nazo bila kuchukua kitu kingine.
Akisimulia zaidi tukio hilo, Kamanda Kalinga alisema Februari 14, mwaka huu Balozi Daraja alimuaga mke wake kuwa anasafiri kwenda Muheza, Tanga na kumuacha na mhudumu wa shamba ambaye alikuwa akiishi kwenye nyumba hiyo.
Alisema wakati Balozi Daraja akiwa safarini, kijana huyo anadaiwa kuwa alimchoma Anna kisu kwenye titi la kushoto na kufa papo hapo.
Alisema mtuhumiwa baada ya kuhakikisha mama huyo amekufa alianza kufanya upekuzi kwenye nyumba hiyo, ikiwemo chumbani kwa balozi.
Alisema mtuhumiwa huyo mara baada ya kuzikuta fedha hizo sehemu zilipokuwa zimehifadhiwa, alitoweka eneo la tukio na kwenda kusikojulikana.
“Nyumba hiyo ilikuwa na vitu vyenye thamani kubwa, lakini inaelekea mtuhumiwa hakuwa na nia navyo, alichukua fedha na kutokomea nazo,” alisema Kamanda Kalinga.
Kamanda Kalinga alisema kuwa upekuzi uliofanywa kwenye chumba cha mtuhumiwa kilichopo nje ya nyumba kubwa ya balozi huyo kulikutwa nguo za aina mbalimbali pamoja na vitu vingine. Alisema nguo hizo ni mali ya mtuhumiwa.
Alisema uchunguzi wa awali uliofanyika kwenye nyumba hiyo, umebaini kuwa mtuhumiwa huyo alifanya kitendo hicho cha kikatili usiku kutokana na mazingira waliyoyakuta.
“Tukio hili lingefanyika mchana huyu mama angepata msaada, lakini inaonyesha wazi kuwa mtuhumiwa alimvizia usiku ndipo akafanya mauaji hayo,” alisema Kamanda Kalinga.
Alisema juhudi za kumsaka mtuhumiwa huyo katika maeneo tofauti jijini Dar es Salaam na nje ya mkoa zinaendelea.
Kamanda Kalinga alisema mtuhumiwa huyo inadaiwa kuwa aliletwa na fundi ujenzi ambaye hajafahamika jina lake kwa ajili ya kazi alizokuwa akizifanya.
Alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa uchunguzi zaidi.
Akizungumza kwa njia ya simu na Nipashe, Balozi Daraja alisema wakati wa tukio la kuuawa kwa mke wake alikuwa safarini mkoani Tanga.
“Jana (juzi) niliporudi nyumbani kutokea Tanga nilipofika kwenye geiti la nyumba yangu, niligonga muda mrefu bila mafanikio,” alisema.
Alisema mara baada ya kufanikiwa kuingia ndani (bila kuelezea aliingiaje), aliukuta mwili wa mke wake ukiwa umelala kwenye gereji huku kisu kikiwa kimechomwa kwenye titi.
Alisema hadi sasa hafahamu mtu aliyefanya kitendo hicho na kwamba uchunguzi unaendelea.
| Comments |
|
3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."
Habari Motomoto
-
Mahakama: Chenge ana kesi ya kujibu Mahakama ya wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam imesema mgombea...
-
Vyama 15 vyasaini rasimu ya mwongozo wa maadili Z`bar Viongozi wa vyama 15 vya siasa jana walisaini rasimu ya mwongozo...
-
Mrufani aongezewa adhabu ya viboko Mahakama ya rufaa Tanzania imemuongea adhabu Mathias Mhagama, aliyepinga...
-
Tanesco yalalamikia vituo bandia vya Luku Shirika la Umeme nchini (Tanesco) limesema kuna ongezeko la vituo...
-
Chadema: Hatutaki siasa za maji taka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema hakina muda...
-
CCM na Chadema Moshi jino kwa jino Mkutano kati ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Lucas Ng’hoboko...
-
Tendwa aiduwaza Chadema Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, ametupilia mbali pingamizi...
-
Chagueni viongozi pasipo kuangalia vyama-Mdee Mgombea ubunge wa jimbo la Kawe kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo...
-
Wanawake wanaougua akili wananyanyasika Wanawake wanaougua ugonjwa wa akili, wananyanyasika kutokana na...
-
Slaa, Dk Bilal uso kwa uso Mwanza Mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),...
-
Mtihani darasa la saba wafanyika kwa utulivu Mtihani wa darasa la saba ulioanza jana kote nchini, ulifanyika katika...
-
Vurugu zaibuka Moshi, Iringa Watu watano wamekamatwa na Polisi mkoani hapa, wakihusishwa na vurugu...
-
Takukuru yapigwa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), imezidi kubanwa...
- 1
- 2
- 3
- 4
- 5
- 6
- 7
- 8
- 9
- 10
- 11
- 12
- 13
- 14
- 15
- 16
- 17
- 18
- 19
- 20
Zilizosomwa Sana
- Schorlaships
- MAJINA YA WANAFUNZI 33658 WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO, VYUO VYA UFUNDI NA CHUO CHA MAJI MWAKA 2010
- United States
- CHAKULA CHA USIKU: WAHANGA SASA NI WANAWAKE! - Mwambie, usione haya
- Dawa za Kuongeza Ufanisi wa Mwanaume Kitandani Zazinduliwa
- AFYA! AFYA! Mambo yote muhimu haya hapa
- Europe
- ***BREAKING NEWS: Watuhumiwa wote kesi ya ZOMBE waachiliwa huru!!!***
- Advertisement Plan
- Australia
- Aliyefumwa akibaka bintiye ala kichapo
- Man Utd ushindi sasa basi
- Ratiba ya Ligi Kuu Uingereza 2010/2011
- Chanjo ya HIV yapunguza maambukizi
- Wanafunzi walioteketea kuzikwa kaburi moja leo
- Japan

