Saturday, July 31, 2010
   
Text Size

Tafuta kwenye Website hii

`Shule za binafsi zipunguze ada`

Wamiliki wa shule za binafsi nchini wameshauriwa kuangalia uwezekano wa kupunguza ada hasa katika kipindi hiki cha mtikisiko wa kiuchumi.

Kufuatia hali hiyo, baadhi ya wazazi wameshaonyesha kushindwa kulipa ada kwa kuwahamisha watoto wao kuotoka shule za Kingereza na kuwarudisha kwenye shule za serikali kufuatia mtikisiko wa kiuchumi.

Ushauri huo ulitolewa jana na Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Shule za Binafsi za Sekondari Kanda ya Dar es Salaam, Kiramu Mbowe, wakati wa maadhimisho ya siku ya Jumiya ya Madola ambayo huadhimishwa Machi 8.

Alisema tayari mtikisiko wa kiuchumi umeshaonyesha matokeo kwenye sekta ya elimu kwani baadhi ya wazazi wameshaonekana wazi kushindwa kulipa ada kitu ambacho lazima wamiliki wa shule binafsi wajadili na kuona namna gani wanaweza kusaidia hasa katika upinguzaji wa ada.

Aidha, alisema maadhimisho ya Siku ya Madola inaweleta wanafunzi na walimu pamoja ambapo wanatumia mada huo kubadilishana mawazo.

Akifungua maadhimisho hayo, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Gaudensia Kabaka, alishukuru uongozi wa shule ya Sekondari ya Shaaban Robert kwa kuandaa maadhimisho hayo ya kitaifa ambayo ni muhimu kwa wanafunzi na watu mbalimbali.

Alisema serikali itaendelea kuinua kiwango cha elimu nchini hasa kwenye upande wa sayansi na teknologia kwa kuongeza fedha kwa mwaka ujao wa fedha.

Makamu wa Rais wa Jumuya ya Madola, Andy Chande, aliwashukuru wazazi wa kuanza kufatilia maendeleo ya watoto wao tofauti na hapo awali walikuwa wakiwaachia walimu peke yao.

Chande alishukuru pia serikali kwa kuendelea kuipa kipaumbele sekta ya elimu hasa kwa mpango wa kuongeza fedha kwa ajili ya kusapoti kauli mbiu ya mwaka huu.


CHANZO: NIPASHE
Comments
Add New Search
Write comment
Name:
Email:
 
Title:
UBBCode:
[b] [i] [u] [url] [quote] [code] [img] 
 
 
Please input the anti-spam code that you can read in the image.

3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."

Habari Motomoto

  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20

Login Form