Saturday, July 31, 2010
   
Text Size

Tafuta kwenye Website hii

EU yaitolea mwito Ugiriki

Umoja wa Ulaya umeitolea mwito Ugiriki kutekeleza hatua inazopanga kuchukua ndani ya siku kadhaa kukabiliana na mgogoro wa fedha ambao umeyatikisa mataifa yanayotumia sarafu ya euro.

Umoja huo pia umeahidi kuisaidia nchi hiyo

kuondokana na tatizo lake la madeni. Akizungumza mjini Hanover, Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel alisema taasisi kadhaa zimeridhika kuwa hatua zitakazochukuliwa na Ugiriki zitafanya kazi.

Aidha, Waziri Mkuu wa Uhispania, Jose Luis Rodriguez Zapatero, amesema matatizo ya Ugiriki yanaweza yakatatuliwa. Bibi Merkel na Zapatero walikuwepo Hanover wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya vifaa vya teknolojia yanayojulikana kama CeBit.

Waziri Mkuu wa Ugiriki Georges Papandreou, anatarajiwa kuwasili Berlin siku ya Ijumaa kukutana na Bibi Merkel, licha ya taarifa kuwa benki ya serikali ya Ujerumani huenda ikashinikizwa kununua dhamana za serikali ya Ugiriki ili kuisaidia nchi hiyo.

Comments
Add New Search
Write comment
Name:
Email:
 
Title:
UBBCode:
[b] [i] [u] [url] [quote] [code] [img] 
 
 
Please input the anti-spam code that you can read in the image.

3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."

Habari Motomoto

  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20

Login Form