Saturday, July 31, 2010
   
Text Size

Tafuta kwenye Website hii

Mpango wa mapinduzi: watu 40 wakamatwa Uturuki.

Waziri Mkuu wa Uturuki Tayyip Erdogan amethibitisha polisi wamewakamata watu 40  wanaohusishwa na njama ya kupanga mapinduzi. Miongoni mwa waliokamatwa ni pamoja na maafisa wa ngazi za juu jeshini.

Erdogan na chama chake cha AK, kilicho na misingi ya dini ya Kiislamu kimekuwa kikizozania madaraka na jeshi la nchi hiyo ambalo halina msingi wowote wa dini pamoja na idara ya mahakama. Chama cha AK kinashtumiwa kutaka kuigeuza Uturuki ifuate maadili ya dini ya Kiislamu.

 

Madai ya njama hiyo ya mapinduzi ni ya tangu mwaka wa 2003, na taarifa za vyombo vya habari zinasema mpango huo ulihusisha kutumia mabomu kuzua hali ya wasiwasi nchini humo, kama kisingizio cha kufanya mapinduzi ya kijeshi.  Jeshi la Uturuki lina historia ya kuingilia siasa Uturuki, tangu mwaka wa 1960 limefanikiwa kuziondoa madarakani serikali nne nchini humo.

Comments
Add New Search
Write comment
Name:
Email:
 
Title:
UBBCode:
[b] [i] [u] [url] [quote] [code] [img] 
 
 
Please input the anti-spam code that you can read in the image.

3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."

Habari Motomoto

  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20

Login Form