Saturday, July 31, 2010
   
Text Size

Tafuta kwenye Website hii

Mgomo wa Lufthansa umesimamishwa.

Ndege za Shirika la ndege la Ujerumani, Lufthansa zimeanza tena safari zake, baada ya marubani wake 4,000 kusimamisha mgomo wao na kurejea kazini usiku wa kuamkia leo. Shirika hilo la Lufthansa lilikuwa limewasilisha ombi mahakamani kusimamisha

mgomo huo wa siku nne.

Chama cha marubani hao Cockpit kikakubali kurejea kazini baada ya kugoma kwa siku moja pekee yake. Makubaliano hayo yanaitisha kuanzishwa kwa majadiliano mara moja na kuzuia kutofanyika kwa mgomo mwingine kabla ya tarehe nane mwezi Machi. Marubani hao wa Lufthansa wanalalamikia kuongezwa mishahara yao kwa asili mia sita pamoja na uhakika wa ajira zao kwa takriban mwaka mmoja.

Hata hivyo, mgomo wa wasimamizi wa mawasiliano ya angani nchini Ufaransa uliopangwa kuanza leo, utaendelea. Vile vileĀ  uwezekano wa kufanyika kwa mgomo wa wahudumu wa ndege za Shirika la Ndege la Uingereza British Airways, itaendelea kutatiza safari za ndege hapa Ulaya.

Comments
Add New Search
Write comment
Name:
Email:
 
Title:
UBBCode:
[b] [i] [u] [url] [quote] [code] [img] 
 
 
Please input the anti-spam code that you can read in the image.

3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."

Habari Motomoto

  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20

Login Form