Saturday, July 31, 2010
   
Text Size

Tafuta kwenye Website hii

Malecela: kuweka mihula kwa wabunge ni kukiuka Demokrasia

Map of Tanzania

Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania ambaye pia ni mbunge wa siku nyingi John Malecela amesema mjadala wa kuweka ukomo kwa wabunge wa Tanzania, waachiwe wananchi ambao ndio wanajua nani anastahili kuwawakilisha.

Malecela ambaye ni miongoni mwa wabunge waliokaa kwa muda mrefu katika bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania amesema kwa ufahamu wake wa siasa za kimataifa hakuna nchi duniani inayoweka ukomo kwa wabunge kukaa madarakani akitolea mfano wa Marekani, Uingereza, Urusi na China.

Malecela amesema katika bunge la sasa la Tanzania karibu asilimia 80 ya wabunge ni vijana na haelewi kauli zinazotolewa kuwa wabunge wengi ni wazee zinatoka wapi. Aliwataka wananchi wanaozungumza hivyo kufanya utafiti wa kina badala ya kuropoka kwenye vyombo vya habari.

Kumekuwa na shinikizo kutoka kwa wadau mbali mbali nchini Tanzania wakitaka kuwepo na ukomo wa kipindi cha ubunge nchini humo, ili kutoa fursa ya mawazo mapya katika bunge hilo, na hasa baada ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo Mizengo Pinda, kusema kuwa yeye anaona kuna umuhimu wa kuwa na ukomo wa mbunge kukaa bungeni.

Comments
Add New Search
Ludovick S Mwijage   |212.242.111.xxx |2010-02-11 03:23:16
Demokrasia ipi Bwana Malecela anayodai hairuhusu ukomo kwa Wabunge (hasa wale
wenye mawazo chakavu na sifa za kifisadi)kukaa madarakani ad nauseam? Mbona
alipokwa Waziri katika serikali ya Awamu ya Kwanza; ya utawala wa madaraka ya
binafsi; hakudiriki kulizungumzia hili la demokrasia ya 'kimataifa?' Na si
kutokana na juhudi za vijana hao, ambao anawarushia katyusha, zilizoiwezesha
Tanzania kurejea tena demokrasia ambayo leo hii Bwana Malecela anajidai kuwa
mtetezi wake? Kama kizazi kipya kilibuni dhana ya kudai demokrasia, iweje
kishindwe kupata nguvu na uwezo wa kuendeleza azma hiyo au kuihami? Kuweka ukomo
kwa Wabunge wa Tanzania kunalenga, kati ya mambo mengine, kuwapa vijana nafasi
(kama walioipata akina Bwana Malecela), kuchati mwelekeo wa Taifa letu na kuzuia
Wabunge mafisadi wasigeuze majimbo wanayoyawakilisha kuwa kama vihamba vyao
binafsi. Wazee ng'atukeni.
Daudi Amiri Mmbaga  - Ngatukeni wazee   |199.175.111.xxx |2010-02-13 03:31:43
Namuunga mkono huyu mzee ukweli tutofautishe siasa na kazi zingine za utendaji
serikalini.Kwasababu ubunge achilia mbali wa kuteuliwa mtu anapata kwa ridhaa ya
wanakura wake sasa ni juu yao wakiona kazeeka basi dawa ni kumpiga chini katika
boksi la kura kama wanaona anafaa na bado ni embe bivu linalofaa kuliwa basi
waendelee kumchagua mpaka nguvu zake zikiisha
Write comment
Name:
Email:
 
Title:
UBBCode:
[b] [i] [u] [url] [quote] [code] [img] 
 
 
Please input the anti-spam code that you can read in the image.

3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."

Habari Motomoto

  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20

Login Form