Thursday, March 11, 2010
   
Text Size

Tafuta kwenye Website hii

Skendo la Ununuzi wa Rada ya Tanzania, BAE Yapigwa Faini Dola Milioni 450


Wakala wa ununuzi wa rada ya Tanzania, Shailesh Vithlani

Skendo la ununuzi wa rada ya ulinzi ya Tanzania toka kwa kampuni ya BAE Systems ya Uingereza limechukua sura nyingine nchini Uingereza kwa kampuni ya BAE kupigwa faini ya dola 450 kwa kukiri kutumia rushwa kukamilisha madili yake.
Kampuni ya BAE System iliyoiuzia rada ya ulinzi Tanzania imepigwa faini ya jumla ya dola Milioni 450 (Zaidi ya Tsh. Bilioni 580) kwa kutumia rushwa katika kukamilisha dili zake na Tanzania, Jamhuri ya Cheki, Hungary na Saudi Arabia.

Awali taasisi ya Kuchunguza Makosa Makubwa ya Jinai (SFO) ya Uingereza iliipa mwezi mmoja BAE Systems kukiri makosa yake au kufikishwa mahakamani

Awali SFO iligundua kuwa mkataba wa ununuzi wa rada wa mwaka 1999, kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Uingereza ya BAE Systems uligubikwa na rushwa kubwa.

Ununuzi wa rada hiyo ulifanikishwa na wakala Shailesh Vithlani ambaye aliifanya Tanzania itoe TSh bilioni 16 zaidi ya bei halisi katika ununuzi wa rada hiyo.

Vithlani inasemekana alipewa dola milioni 12 (zaidi ya TSh. bilioni 12) kama kamisheni ya kufanikisha dili hilo na inasemekana aligawana pesa hizo na maafisa saba wa ngazi za juu katika serikali ya Tanzania.

Vithlani alitoroka Tanzania miaka mitatu iliyopita akiwa nje kwa dhamana baada ya kufunguliwa mashtaka na alikamatwa mwaka jana nchini Uswizi alikokuwa akijificha.

Mbali na rushwa kutumika katika ununuzi wa rada ya Tanzania, BAE pia ilituhumiwa kutumia rushwa katika kukamilisha uuzaji wa ndege moja ya kijeshi kuiuzia nchi ya Afrika Kusini na uuzaji wa ndege nyingine ya kijeshi ambao haukufanikiwa kwa Jamhuri ya Cheki.

"Kampuni ya BAE inajutia yaliyotokea na inakubali kubeba mzigo kwa matatizo yaliyotokea", alisema mwenyekiti wa BAE, Dick Olver.

BAE ilikiri kuwa malipo ya kamisheni kwa mtekelezaji wa dili la rada ya Tanzania hayakuwekwa wazi kama ilivyotakiwa na kwasababu hiyo BAE imekubali kutoa paundi milioni 30 ambazo baadhi ya pesa hizo zitatumika kwaajili ya manufaa ya Tanzania.

Mkurugenzi wa SFO, Richard Alderman alielezea kufurahishwa kwake na makubaliano yaliyofikiwa na kuongeza kuwa huo ndio utakuwa mwisho wa uchunguzi wao kwa kampuni ya BAE.
Comments
Add New Search
Anonymous   |196.201.151.xxx |2010-02-10 13:17:00
Ndugu WaTanzania,jambo hili lilifahamika mda mfupi baada ya lada kununuliwa ila
tuu kwa sababu nchi yetu ni sawa na baba anae fanya dili na watu kuja kununua
debe moja pekee la maharage tulilonalo nyumbani ili baada ya hapo watoto wafe
njaa na baba hiyo pesa huenda kunywa kayoga,Hili lilitakiwa kuwa
lilishachukuliwa hatua mda mrefu,ila tuu mimi sina maoni ila nina
masaawali.
1.Hao viongozi wa juu wa serikali walioshiriki na huyo gabacori ni
akina nani?????? watajwe majina na wapelekwe mahakamani.
2.Hiyo faini ambayo
BAE wamepigwa jee hiyo fedha inalipwa Tanzania au inakwenda wapii????
3.Kama
siyo Tanzania inalipwa,jee Serikali inampango gani kuchukua hatua za kisheria
kwa BAE kwa kuiingiza Mkenge na lada ambyo haikuweza hata kufanya kazi kwa siku
moja.
mwisho:
Ninatamani waTanzania tungepew nafasi ya kuwahukumu hao
waliotuingiza mkenge wakati kuna Walimu mashuleni hawana mishahara na madactar
pia wgonjwa wasiowe...
Write comment
Name:
Email:
 
Title:
UBBCode:
[b] [i] [u] [url] [quote] [code] [img] 
 
 
Please input the anti-spam code that you can read in the image.

3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."

Habari Motomoto

  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20

Login Form