Mtoto wa Miaka 9 Ajifungua Mtoto
![]() |
Msichana mwenye umri wa miaka 9 wa nchini China ameingia kwenye rekodi ya akina mama wenye umri mdogo sana duniani baada ya kujifungua mtoto wa kike mwenye uzito wa kilo 2.7. |
|
| Msichana huyo mwanafunzi mwenye umri wa miaka 9 alijifungua mtoto wake wa kike kwenye hospitali moja katika mji Changchun, katika jimbo la Jilin nchini China. Msichana huyo alijifungua mtoto huyo kwa njia ya operesheni wakati mimba yake ikiwa na muda wa miezi minane na nusu. Gazeti la The City Evening News la nchini China limeripoti kuwa msichana huyo na mwanae wote wana afya njema hivi sasa lakini wazazi wa msichana huyo wamepeleka malalamiko yao polisi. Kwa mujibu wa sheria za China, kujamiiana na mtoto mwenye umri chini ya miaka 14 kunahesabika kama kosa la ubakaji. Msichana huyo wa China ameingia kwenye orodha ya akinana mama wa duniani wenye umri mdogo sana. Msichana mwenye umri mdogo kuliko wote duniani kujifungua mtoto ni Lina Medina, wa nchini Peru, ambaye alijifungua mtoto akiwa na umri wa miaka mitano mwaka 1939. Serikali ya China imekuwa ikiendesha kampeni nchi nzima kupunguza idadi ya mimba katika umri mdogo kwa kuzipiga marufuku tovuti zote zenye picha au video za ngono. Wanafunzi wa shule za sekondari wamekuwa wakisimamishwa shule wanapogundulika wanajihusisha na vitendo vya ngono. Hata hivyo kumekuwa na ongezeko kubwa la wanafunzi wanaotoa mimba kiasi cha kwamba hospitali moja ya mjini Shanghai ilisema kuwa theluthi ya wanawake wanaotoa mimba kwenye hospitali hiyo ni wanafunzi. |
||
| Comments |
|
Powered by !JoomlaComment 3.26
3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."
Habari Motomoto
-
Jengo la Ubalozi wa Tanzania nchini Nigeria lahitaji bilioni 4/- Ubalozi wa Tanzania nchini Nigeria, unahitaji jumla ya Shilingi bilioni...
-
Mwalimu aliyefariki aendelea `kula` mshahara, apanda cheo Halmashauri ya wilaya ya Bunda, imeingia kwenye kashfa kubwa baada...
-
EAC kujenga mtandao wa reli Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, zimeazimia kujenga mtandao wa...
-
Tanroads yaanzisha mchakato wa mradi wa mabasi ya kasi Hatimaye Wakala wa Barabara nchini (Tanroads), umetangaza nia ya kutekeleza...
-
RCO atoa ushahidi kesi ya wizi NMB Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa kipolisi wa Ilala (RCO), Duani Nyanda...
-
Ngeleja: Serikali kununua Dowans ndoto Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, amekanusha vikali kwamba...
-
Kikwete Rais wa kwanza kutia mguu Kitunda Ziara ya Rais Jakaya Kikwete kwenye kata ambayo haijawahi kutembelewa...
-
Ikulu lawamani vita ya ufisadi RIPOTI ya Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mpango wa Kutathmini Utawala...
-
Jaji Bomani kutopambana na Rais Kikwete 2010 BAADA ya kutajwa kuwa na dhamira ya kumvaa Rais Jakaya Kikwete, kwenye...
-
Kapuya, Tucta washangaana SERIKALI imesema inafanya uchunguzi kujua sababu zilizofanya Shirikisho...
-
Benki ya Dunia yatoa mikopo ya nyumba ya Sh50 bilioni BENKI ya Dunia (WB) imeidhinisha Tanzania kupatiwa mkopo wa dola za...
-
Watu 3,000 wapiga simu kujua kama Maalim Seif amekufa ZAIDI ya watu 3,800 wamepiga simu kutoka kona mbalimbali duniani kwa...
-
Marekani yaonya wingi wa bidhaa feki nchini BALOZI wa Marekani nchini , Alfonso Lenhardt amesema biashara ya bidhaa...
- 1
- 2
- 3
- 4
- 5
- 6
- 7
- 8
- 9
- 10
- 11
- 12
- 13
- 14
- 15
- 16
- 17
- 18
- 19
- 20
Zilizosomwa Sana
- Schorlaships
- Advertisement Plan
- AFYA! AFYA! Mambo yote muhimu haya hapa
- CHAKULA CHA USIKU: WAHANGA SASA NI WANAWAKE! - Mwambie, usione haya
- Aliyefumwa akibaka bintiye ala kichapo
- Dawa za Kuongeza Ufanisi wa Mwanaume Kitandani Zazinduliwa
- United States
- ***BREAKING NEWS: Watuhumiwa wote kesi ya ZOMBE waachiliwa huru!!!***
- Europe
- Man Utd ushindi sasa basi
- Wanafunzi walioteketea kuzikwa kaburi moja leo
- Google now in Tanzania, Advertise!
- Australia
- Henry Joseph Shindika aula
- Vyeti feki - Mawaziri sita wanasa
- United Kingdom


