Cheyo, Chenge waingia vitani
Mbunge wa zamani wa Bariadi Magharibi, Isaac Cheyo, amemtumia salama mbunge wa sasa wa jimbo hilo, Anderw Chenge, kwamba wakati wa kuachia ngazi umewadia kwa sababu mwenye jimbo lake anawasili.
Cheyo ambaye ni Katibu Mwenezi Taifa wa Chama cha United Democratc Party (UDP), alisema anajipanga kikamilifu kulirejesha jimbo hilo mikononi mwa UDP, baada ya kulipoteza mwaka 2005 kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Chenge ambaye mara tu alipochaguliwa aliteuliwa kuwa Waziri wa Afrika Mashariki na baadaye Waziri wa Miundombinu, baada ya Baraza la Mawaziri kuundwa upya Februari, 2008, lakini alijiuzulu kwa sababu ya sakata ya rada.
Mbunge huyo ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, hakudumu katika nafasi hiyo baada kufichuliwa kwa kashfa ya kukutwa akimiliki akaunti yenye fedha zinazohusishwa na rushwa katika ununuzi wa rada, huku akiwa hajatangaza kumiliki hazina hiyo katika fomu za kutangaza mali kwa kamishna wa maadili.
Chenge anatuhumiwa kuwa akiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) wakati wa uongozi wa awamu ya tatu, alihusika katika kashfa hiyo, ambapo rada ya kijeshi ilinunuliwa kwa kiasi kikubwa cha fedha tofauti na thamani yake halisi kutoka Uingereza, licha ya Uingereza kuitahadharisha Tanzania isiinunue rada hiyo.
Fedha za Chenge, Dola milioni 1 (Sh. bilioni 1.2) zilikutwa kwenye akaunti yake katika benki moja iliyoko katika kisiwa cha Jersey, Uingereza.
Chenge alikanusha kuhusika katika rushwa hiyo na alisema fedha zake ni mapato halali kutokana na kazi yake ya uanasheria na urithi wa familia yake.
Rada hiyo iliyonunuliwa kwa Sh. bilioni 40 kiasi cha Sh bilioni 12 zilidaiwa kugawanywa kama rushwa kwa watu mbalimbali, wakiwamo viongozi waandamizi wa Tanzania, baadhi wakitajwa kuwa ni Chenge na aliyekuwa gavana wa Benki Kuu wakati huo, Dk. Idris Rashidi
Akizungumza na Nipashe jana Cheyo ambaye alibwagwa katika uchaguzi mkuu oktoba 2005 na Chenge, alisema amejipanga kikamilifu kumbwaga Chenge katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika huu kwa kile alichodai kuwa jimbo hilo sasa limedumaa na kukosa maendeleo, hali ambayo alidai kuwa wapiga kura wake waliitarajia.
Cheyo ambaye ametangaza nia yake ya kugombea tena ubunge, alitamba kuwa jimbo hilo alimwachia Chenge ambaye pia ni ndugu yake kiukoo baada ya yeye kujielekeza katika mambo ya biashara za mazao ya chakula ndani na nje ya nchi.
Cheyo alitamba na kusema kuwa ushindi wa CCM katika jimbo hilo mwaka 2005 ni sawa na kumwazima suti bwana harusi na baada ya kufunga ndoa na bi harusi sharti airejeshe suti hiyo kwa mwenyewe ambaye yeye (Cheyo).
Alisema kuwa wananchi wa jimbo hilo wamemwomba agombee tena kiti hicho kwa kile alichodai kuwa UDP kimewaletea maendeleo licha ya kukiri kuwa chama tawala CCM ndicho kilichotekeleza baadhi ya miradi ya maendeleo jimboni humo.
Cheyo aliyeliongoza jimbo hilo kuanzia mwaka 1995-2005, alisema:
“Ninakwenda kulirejesha jimbo langu kwa mwenye suti, mwaka 2005 nilimwazima Chenge hiyo suti ya ubunge kama unavyomuazima bwana harusi asiye kuwa na vazi katika kufunga ndoa yake.
“Hilo ni jimbo langu na ushindi ni wazi kwangu na chama changu cha UDP chenye itikadi ya “upendo na utajirisho”, alisema mwanasiasa huyo ambaye ni mdogo wake Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo (UDP).
Cheyo alisema kuwa wananchi wa jimbo hilo wamejionea wenyewe jinsi upinzani kutoka UDP ulivyowasaidia kuwaletea maendeleo katika kipindi cha mwaka 1995 hadi 2005 licha kuwa miradi mingi imetekelezwa na chama tawala ikiwemo ile ya sekta za elimu, afya, maji na miundombinu wilayani Bariadi.
Chama cha UDP kimekuwa kikitoa ushindani mkubwa mkoani hapa hususani Wilaya ya Bariadi na maeno mengine ya Meatu hasa jimbo la Kisesa.
Hivi karibuni, Mwenyekiti wa chama hicho, John Cheyo katika salamu zake kwa wananchi mbele ya Rais Jakaya Kikwete katika ziara yake mkoani Shinyanga mwezi uliopita, alitamba mbele ya wananchi kuwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu UDP nao wapo akimaanisha kuwa watahakikisha wanaendeleza kunyakua viti vingi vya udiwani na hata ubunge.
Katika hotuba yake fupi muda mfupi tu baada ya Rais Kikwete kufungua daraja la mto Simiyu Januari 19, mwaka huu, Cheyo alisema kuwa pamoja na CCM kutekeleza ahadi zake kwa wananchi ikiwemo ujenzi wa daraja hilo, bado mwenyekiti huyo alitamba kuwa wananchi wana imani na chama cha UDP na kuongeza kuwa watakichagua katika uchaguzi wa mwaka huu.
| Comments |
|
|
||||||||||||
3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."
Habari Motomoto
-
Wahariri kujadili jinsi ya kuwasaidia wapiga kura wakati wa kampeni Wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini watakutana jijini...
-
Slaa apata mapokezi makubwa Musoma, Mwanza Maelfu ya wananchi, wakiwamo watumishi wa serikali, wafanyabiashara...
-
Jaji Mkuu: Hatukushinikizwa hukumu ya mgombea binafsi Jaji Mkuu wa Tanzania, Augustine Ramadhan, amesema uamuzi wa Mahakama...
-
Ajali ya basi yaua abiria 16 Watu 16 wamefariki dunia na wengine 48 kujeruhiwa baada ya basi la...
-
Kura ya maoni Z`bar yamg`oa DC Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, amemfukuza kazi Mkuu wa Wilaya...
-
Takukuru sasa inatawala nchi Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imewakamata makada...
-
Karume awa mbogo Z`bar Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume, amevunja ukimya kwa kusema kuwa...
-
Umati wamlaki Slaa jijini Arusha Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod...
-
Jaji Eliamani Mbise afariki dunia Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Eliamani Mbise, amefariki dunia...
-
Tume ya uchaguzi yataka ushahidi wizi wa kura Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeomba kupewa taarifa za mianya ya wizi...
-
Waibuka washindi Viti Maalum CCM Wagombea kadha wameibuka na ushindi katika mchuano wa kura za uteuzi...
-
Waziri Sitta azungumzia sakata ya Takukuru Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Magreth Sitta, amekanusha...
-
Kamanda Takukuru ashushwa cheo WAKATI habari za rushwa zikiendelea kutawala harakati za kuwania ...
- 1
- 2
- 3
- 4
- 5
- 6
- 7
- 8
- 9
- 10
- 11
- 12
- 13
- 14
- 15
- 16
- 17
- 18
- 19
- 20
Zilizosomwa Sana
- Schorlaships
- MAJINA YA WANAFUNZI 33658 WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO, VYUO VYA UFUNDI NA CHUO CHA MAJI MWAKA 2010
- United States
- CHAKULA CHA USIKU: WAHANGA SASA NI WANAWAKE! - Mwambie, usione haya
- AFYA! AFYA! Mambo yote muhimu haya hapa
- Dawa za Kuongeza Ufanisi wa Mwanaume Kitandani Zazinduliwa
- Europe
- Advertisement Plan
- ***BREAKING NEWS: Watuhumiwa wote kesi ya ZOMBE waachiliwa huru!!!***
- Aliyefumwa akibaka bintiye ala kichapo
- Australia
- Man Utd ushindi sasa basi
- Wanafunzi walioteketea kuzikwa kaburi moja leo
- Chanjo ya HIV yapunguza maambukizi
- United Kingdom
- Henry Joseph Shindika aula

