Saturday, July 31, 2010
   
Text Size

Tafuta kwenye Website hii

Vyuo 64 vya uuguzi havijasajiliwa

Takriban vyuo 64 vya wakunga na wauguzi jijini Dar es Salaam na baadhi ya mikoa, havijasajiliwa.

Aidha, vyuo hivyo vimekuwa vikiwatumia wanafunzi wa sekondari wa mchepuo wa sayansi kuwafundisha wakunga na wauguzi.

Kauli hiyo ilitolewa na Msajili wa Baraza la Wakunga na Wauguzi, Gustav Moyo, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.

Alisema vyuo hivyo havina walimu wenye taaluma hali inayosababisha viwatumie wanafunzi wa sekondari wa michepuo ya sayansi kufundisha.

Moyo alisema vyuo hivyo vipo katika Manispaa za Ilala, Temeke na Kinondoni na vingine vipo mikoani.

Aliwataka wananchi kwenda wilayani kuulizia vyuo vilivyosajiliwa badala ya kwenda kwenye vyuo visivyo na sifa kwani kufanya hivyo ni kupoteza fedha na muda.

Aidha, alisema aliyesoma katika vyuo hivyo visivyo na usajili hawezi kusajiliwa na Baraza.

 

CHANZO: NIPASHE
Comments
Add New Search
Write comment
Name:
Email:
 
Title:
UBBCode:
[b] [i] [u] [url] [quote] [code] [img] 
 
 
Please input the anti-spam code that you can read in the image.

3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."

Habari Motomoto

  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20

Login Form