Saturday, July 31, 2010
   
Text Size

Tafuta kwenye Website hii

Mafundi ujenzi wafa kwa kufunikwa kifusi D`Salaam

Mafundi ujenzi wawili wakazi wa Gongo la Mboto, jijini Dar es Salaam, wamekufa papo hapo baada ya kufunikwa na kifusi cha mchanga walichokuwa wakikichimba.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile, alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi eneo la Pugu Bagdad.

Kamanda Shilogile alisema mafundi hao ambao ni James Katenga (27) na Adamu Mtolela (30), walikutwa na umauti huo wakati wakiendelea na uchimbaji mchanga kwenye moja ya machimbo yaliyopo eneo hilo.

Wakati huohuo, dereva wa pikipiki Mussa Issah (24), amekufa papo hapo na abiria wake kujeruhiwa vibaya baada ya kugongwa na gari dogo aina ya Audi Saloon eneo la Brush lililopo barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Liberatus Sabas, alisema ajali hiyo ilitokea juzi eneo hilo wakati gari hilo lenye namba za usajili T 357 ASE likiendeshwa na Magreth Lega (34).

Alisema gari hilo lilikuwa alikitokea eneo la Kamata kuelekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakati dereva wa pikipiki hiyo yenye namba za usajili T 391 AYU alikuwa akitokea Tazara kuelekea Kamata.

Kamanda Sabas alimtaja aliyejeruhiwa katika ajali hiyo kuwa ni Gidmash Geofrey (22), ambaye amelazwa hospitali ya Temeke kwa matibabu na dereva wa gari hilo anashikiliwa na polisi wakati uchunguzi wa tukio hilo ukiendelea.

 

CHANZO: NIPASHE
Comments
Add New Search
Write comment
Name:
Email:
 
Title:
UBBCode:
[b] [i] [u] [url] [quote] [code] [img] 
 
 
Please input the anti-spam code that you can read in the image.

3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."

Habari Motomoto

  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20

Login Form