Shahidi kesi ya Liyumba ashindwa kutoa ushahidi
MKURUGENZI wa ukaguzi wa miradi kutoka Wizara ya Fedha na Uchumi, Amir Mcharo jana aliiomba mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu asitoe ushahidi katika kesi inayomkabili kigogo wa zamani wa Benki Kuu (BoT), Amatus Liyumba kwa madai kuwa anasumbuliwa na shinikizo la damu.
Mcharo, 48, ambaye ni shahidi wa tisa wa upande wa mashtaka alitoa ombi hilo jana mbele ya jopo la mahakimu watatu linaloongozwa na Edson Mkasimongwa mara baada ya kuapishwa na kupanda kizimbani tayari kwa kutoa ushahidi.
Liyumba anakabiliwa na kesi ya kuisababishia serikali hasara ya Sh221 bilioni wakati wa mradi wa ujenzi wa majengo ya ghorofa pacha yaliyo kwenye viwanja vya ofisi ya makao makuu ya BoT.
Mara baada ya kutoa ombi hilo, Hakimu Mkasimongwa alimuuliza shahidi huyo kuwa kama ugonjwa wake hautokani na msongo wa mawazo au hofu ya kutoa ushahidi.
Lakini shahidi huyo alikataa akisema kuwa huwa anasumbuliwa na ugonjwa huo mara kwa mara.
"Naomba nisitoe ushahidi leo (jana), kesho nikiwa najisikia vizuri nitakuja kutoa ushahidi wangu, "aliomba shahidi huyo.
Wakili wa Liyumba, Majura Magafu alidai kuwa kila mtu ana shinikizo la damu hivyo kwa kuwa shahidi huyo alishasimama kizimbani, akaapishwa hana budi kutoa ushahidi angalau kidogo.
Magafu alidai lazima ifike wakati upande wa mashtaka uelewe shahidi huyo anaposema ana shinikizo la damu kwa kuwa hata mteja wao ana magonjwa yake na bado yupo mahabusu.
Baada ya kutolewa kwa hoja hizo, Hakimu Mkasimongwa aliamuru leo upande wa mashtaka ufike mahakamani na mashahidi wao wote, akiwepo mkurugenzi huyo wa ukaguzi wa miradi.
CHANZO MWANANCHI
| Comments |
|
3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."
Habari Motomoto
-
Wahariri kujadili jinsi ya kuwasaidia wapiga kura wakati wa kampeni Wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini watakutana jijini...
-
Slaa apata mapokezi makubwa Musoma, Mwanza Maelfu ya wananchi, wakiwamo watumishi wa serikali, wafanyabiashara...
-
Jaji Mkuu: Hatukushinikizwa hukumu ya mgombea binafsi Jaji Mkuu wa Tanzania, Augustine Ramadhan, amesema uamuzi wa Mahakama...
-
Ajali ya basi yaua abiria 16 Watu 16 wamefariki dunia na wengine 48 kujeruhiwa baada ya basi la...
-
Kura ya maoni Z`bar yamg`oa DC Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, amemfukuza kazi Mkuu wa Wilaya...
-
Takukuru sasa inatawala nchi Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imewakamata makada...
-
Karume awa mbogo Z`bar Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume, amevunja ukimya kwa kusema kuwa...
-
Umati wamlaki Slaa jijini Arusha Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod...
-
Jaji Eliamani Mbise afariki dunia Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Eliamani Mbise, amefariki dunia...
-
Tume ya uchaguzi yataka ushahidi wizi wa kura Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeomba kupewa taarifa za mianya ya wizi...
-
Waibuka washindi Viti Maalum CCM Wagombea kadha wameibuka na ushindi katika mchuano wa kura za uteuzi...
-
Waziri Sitta azungumzia sakata ya Takukuru Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Magreth Sitta, amekanusha...
-
Kamanda Takukuru ashushwa cheo WAKATI habari za rushwa zikiendelea kutawala harakati za kuwania ...
- 1
- 2
- 3
- 4
- 5
- 6
- 7
- 8
- 9
- 10
- 11
- 12
- 13
- 14
- 15
- 16
- 17
- 18
- 19
- 20
Zilizosomwa Sana
- Schorlaships
- MAJINA YA WANAFUNZI 33658 WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO, VYUO VYA UFUNDI NA CHUO CHA MAJI MWAKA 2010
- United States
- CHAKULA CHA USIKU: WAHANGA SASA NI WANAWAKE! - Mwambie, usione haya
- AFYA! AFYA! Mambo yote muhimu haya hapa
- Dawa za Kuongeza Ufanisi wa Mwanaume Kitandani Zazinduliwa
- Europe
- Advertisement Plan
- ***BREAKING NEWS: Watuhumiwa wote kesi ya ZOMBE waachiliwa huru!!!***
- Aliyefumwa akibaka bintiye ala kichapo
- Australia
- Man Utd ushindi sasa basi
- Wanafunzi walioteketea kuzikwa kaburi moja leo
- Chanjo ya HIV yapunguza maambukizi
- United Kingdom
- Henry Joseph Shindika aula

