Saturday, July 31, 2010
   
Text Size

Tafuta kwenye Website hii

Serikali yaandaa bajeti ya ziada

Serikali inakusudia kuongeza kiasi cha Sh. bilioni 19 katika bajeti yake ya mwaka huu ambacho pamoja na mambo mengine, kitatumika kusaidia sekta ya kilimo kwa kutoa mikopo kwa wakulima kupitia Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB).

Muswada wa kuidhinisha nyongeza hiyo ambao umepangwa kujadiliwa na wabunge kwa siku mbili mfululizo kuanzia leo, utaingizwa kwenye bajeti ya Wizara ya Fedha na Uchumi.

“Itakumbukwa kuwa katika hotuba ya Rais Jakaya Kikwete ya Agosti 21, mwaka 2008, alielekeza kwamba fedha za Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania, zitakazorudishwa serikalini ziingizwe katika mfuko mkuu wa Serikali kwa ajili ya matumizi ya shughuli za maendeleo ya nchi ikiwemo kuongeza fedha kwenye mfuko wa ruzuku ya mbolea,” inasomeka sehemu ya muswada huo.

Wakati huo huo, baadhi ya wafadhili wamejitoa kuchangia bajeti ya mwaka huu na wengine wamekataa kutoa kiasi chote cha fedha walichokuwa wameahidi.

Akitoa mwongozo wa bajeti ijayo bungeni jana, Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, alisema Uholanzi imetangaza kusitisha msaada wake wa dola za Kimarekani milioni 40.

Alisema Uingereza imesitisha kutoa kiasi cha paundi milioni 10 ambazo ni zaidi ya Sh. bilioni 20 wakati Denki ya Dunia imesitisha mchango wa dola milioni 10.

Alisema hadi Desemba mwaka jana, Japan na Ujerumani hazikuwa zimetoa kiasi chochote cha ahadi zao kwenye bajeti ya Serikali.

Alisema wamesitisha kutoa fedha hizo kwa maelezo kuwa hawaridhishwi na juhudi za Tanzania katika kuboresha mazingira ya biashara.

 

CHANZO: NIPASHE
Comments
Add New Search
Write comment
Name:
Email:
 
Title:
UBBCode:
[b] [i] [u] [url] [quote] [code] [img] 
 
 
Please input the anti-spam code that you can read in the image.

3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."

Habari Motomoto

  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20

Login Form