Thursday, March 11, 2010
   
Text Size

Tafuta kwenye Website hii

Rais Mutharika wa Malawi, mwenyekiti mpya wa AU

Kiongozi wa Libya Muamar Gadhafi ameshindwa katika juhudi zake za kutaka kuongeza muda wake kama mwenyekiti wa Umoja wa Afrika. Katika mkutano wa viongozi na marais wa Umoja huo wenye wanachama 53 ulioanza leo,

mjini Addis Ababa Ethiopia, rais Bingu wa Mutharika wa Malawi alichaguliwa kuwa  mwenyekiti mpya.

Utawala wa mwaka moja wa Gadhafi uligubikwa na wazo lake la kuwa na Muungano wa nchi za  Afrika. Katika mkutano huo, Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameshutumu  vikali  tabia inayoshika kasi Afrika ya watu kuchukua madaraka kwa nguvu. Ban Ki-moon alisema kuingia madarakani kwa serikali kadhaa Afrika kinyume cha katiba ni mtindo unaotia wasiwasi.

Bara la Afrika limekabiliwa na mizozo kadhaa ya kisiasa, kama kisiwa cha Madagascar, Mauritania na yale mauaji ya wafuasi wa upinzani huko Guinea na mzozo unaoendelea nchini Sudan.

Comments
Add New Search
mutalemwa  - huyu jamaa kazoea   |212.165.169.xxx |2010-02-03 06:09:05
Huyu kiongozi hajui demokrasia, katawala nchiyake kwa mda mrefu, hivyo alifikiri
atabaki milele kwenye madaraka ya AU, jamani viongozi tueshimu sheria
zilizowekwa, kama tuna mda wetu unaisha wa kuongoza, hatuna budi kuondoka
madarakani.
BLACKMANNEN   |194.237.142.xxx |2010-02-03 22:50:45
Wewe "mutalemwa", kama mtu hujui kitu ni vema kukaa kimya. Propaganda za
mataifa tajiri zenye nia ya kutusambaratisha Umoja wetu wa Waafrika wewe
zimekutawala kichwani mwako.
Gaddafi amekuwa mstari wa mbele kuunganisha Bara
la Afrika tangu siku nyingi. Na mataifa tajiri yanamwona ni mtu hatari kwa
sababu hiyo, ni lazima yamseme vibaya, ili watu kama ninyi mrukie treni bila
kujua iendako.
"mutalemwa", pilipili iliyo shambani wewe inakuwashia
nini? Wananchi wa Libya hawajasema kuwa wamechoka kuongozwa na Gadaffi, wala
wewe mutalemwa huijui katiba ya Libya inasema nini kuhusu ukomo wa viongozi wa
nchi hiyo. Kwa hiyo usiwasemee Walibya. Katiba ya nchi yako sio sawa na nchi
zingine. Habari ndiyo hiyo!!!
katarina   |78.41.229.xxx |2010-02-04 07:27:50
ni sawa kabisa blackman ni vizuri kujua mtazamo wa wengi huwani tofauti na
wachache kwani hawaelewi mbinu na lengo la mataifa tajiri.gadafi amekuwa mtu
mwenye kusimamia anachoamini anonekan mkorofi kwa sababu amekuwa anawazibia ama
kuwaharibia mataifa tajiri katika kuuendelea kututawala na kutupangiapangia
mambo yao yeye gadafi anafanya anayoyafanya kwa hali yoyote ile kwa manufaa ya
watu wake na nchi yake.which is good and desired.hata obana alisema wakati
mwingine yakupasa kutumia mabavu kupata unachotaka kwa maslai ya wananchi
wako.gadafi is good leader who knows wat is right no matter wat.who said
democracy is best in leading anyway.tafakarini
Write comment
Name:
Email:
 
Title:
UBBCode:
[b] [i] [u] [url] [quote] [code] [img] 
 
 
Please input the anti-spam code that you can read in the image.

3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."

Habari Motomoto

  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20

Login Form