Wednesday, March 10, 2010
   
Text Size

Tafuta kwenye Website hii

China kuziwekea vikwazo kampuni za Marekani

Wizara ya mambo ya nchi za nje ya China imesema nchi hiyo, itaziwekea vikwazo kampuni za Marekani zilizohusika katika biashara ya kuiuzia Taiwan silaha zilizogharimu dola bilioni 6.4.  Kampuni ambazo huenda

zikaathirika, ni  pamoja  na  kampuni  ya  kuunda ndege  Boeing pamoja na United Technologies, kampuni hizo mbili zina  maslahi makubwa ya kibiashara nchini China.

Naibu  waziri wa nchi za nje wa China, He Yafei amewasilisha malalamiko  rasmi kwa balozi wa Marekani nchini China, Jon Huntsman akisema biashara hiyo ya silaha itaathiri sehemu  kubwa  ya  uhusiano wa nchi hizo mbili. Mshauri mkuu wa rais Obama Generali James Jones hata hivyo amesema uhusiano kati ya Marekani na China ni madhubuti na hauwezi kuathirika  kutokana na biashara hii ya silaha.

Uamuzi wa Marekani wa kuiuzia Taiwan makombora ya kujikinga na helkopta za kijeshi imeibua mvutano mkubwa kati ya nchi hizo mbili, na China imeamua kusitisha kwa muda ushirikiano wa kijeshi na Marekani na pia kufutilia mbali kwa sasa majadiliano kuhusiana na mkakati wa usalama pamoja na kudhibitiwa kwa silaha.

Comments
Add New Search
Write comment
Name:
Email:
 
Title:
UBBCode:
[b] [i] [u] [url] [quote] [code] [img] 
 
 
Please input the anti-spam code that you can read in the image.

3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."

Habari Motomoto

  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20

Login Form