Saturday, July 31, 2010
   
Text Size

Tafuta kwenye Website hii

Dawa za Kuongeza Ufanisi wa Mwanaume Kitandani Zazinduliwa




Tatizo la wanaume kuwahi kufika kileleni mapema ambalo huzua hofu kwa wanaume wengi sana duniani kiasi cha wengine kwenda kwa waganga kutafuta tiba limepatiwa ufumbuzi baada ya dawa ambayo inasemekana inaongeza ufanisi mara tatu zaidi kuzinduliwa nchini Ufaransa.
Tatizo la wanaume kuwahi kufika kileleni mapema wakati wa kujamiiana ambalo huwatia hofu mamilioni ya wanaume wengi duniani limepatiwa dawa kwa mara ya kwanza.

Tatizo hili huwanyima raha wanaume wengi kwani mwanaume anapowahi kufika kileleni mapema kabla ya mpenzi wake humwacha mwanamke akiwa bado hajafikia hitimisho la raha ya kujamiiana.

Wanaume wenye tatizo hili ili wasiaibike kitandani mbele ya wapenzi wao wamekuwa wakihaha kutafuta dawa za kuwafanya waweze kuwaridhisha wapenzi wao, kuna wanaume wengine hufikia hatua za kwenda kwa waganga kutafuta tiba.

Dawa za kutibu tatizo hilo zimezinduliwa kwenye kongamano la tatu la matibabu ya magonjwa ya jinsia linalofanyika nchini Ufaransa.

Dawa hizo mpya ambazo zimepewa jina la "Priligy" zimetengenezwa kwa kutumia madawa ya Dapoxetine ambayo yamegundulika kuonyesha ufanisi mkubwa katika kuchelewesha mwanaume kufika kileleni mapema.

Wanaume waliotumia dawa hizo wakati wa majaribio ufanisi wao kitandani unasemekana uliongezeka kwa mara tatu zaidi.

Dawa hizo zimethibitishwa rasmi ufanisi wake na vyombo vya afya nchini Austria, Finland, Ujerumani, Italia, Hispania, Sweden na Ureno.

Prof. Jacques Buvat wa taasisi iliyovumbua dawa hizo alisema kuwa dawa zinaweza zikatumiwa na wanaume wenye umri kati ya miaka 18 na 64 na hazina madhara yoyote katika kusimama kwa uume.

Prof Buvat alisema kuwa wanaume wengi hufika kileleni kati ya dakika moja na dakika kumi. " Kwa wastani muda unaokubalika ni kati ya dakika nne na tano, wanaume wanaofika kileleni ndani ya dakika moja au chini ya dakika moja huhesabika wana tatizo la kufika kileleni mapema".

"Tatizo la wanaume kuwahi kufika kileleni mapema huwatokea wanaume wengi zaidi kuliko tatizo la kusimama vyema kwa uume".

"Wanaume wengi huwa hawapendi kuzungumzia tatizo hili na asilimia 40 ya wanaume hutumia pombe kama njia ya kutatua tatizo hilo" alisema.
Comments
Add New Search
matley  - banker   |196.43.64.xxx |2009-08-17 09:18:45
du hii kali maana midume mingi tunajifanya wababe wa ngumi inapokuja ishu ya ku
do ndo msala
Akyoo   |41.220.128.xxx |2009-08-18 08:02:30
Do, ndio kusema Arusha dawa zenyewe zimefika?
mavusha  - do   |41.222.176.xxx |2009-08-20 10:40:48
hii kali ya mwaka.

ila ni nzuri tujitahidi zije tz.
EMMANUEL   |196.43.65.xxx |2009-08-21 06:50:36
wala haina kipingamizi,this is real a problem to most of we-men, hope to receive
hem with a cheerful smile, IMMANUEL
kyoro  - Good   |212.247.71.xxx |2009-08-27 09:15:58
ili Mwana ume asifike kwa haraka kileleni nilazima awe na mazoezi ya msuli wa
PC. kama itashindikana hivyo then anaweza akatumia dawa but madawa maera nyingin
yana madhara mengi sana ikiwa ni pamoja kupungukiwa nguvu kabaya wakati wa uzee
wenyewe kufika
pam  - dawa za kuongeza nguvu   |196.44.163.xxx |2009-12-01 03:41:16
masuala ya madawa ni unazungumzia sumu. Dawa yeyote ina madhara kwa kutumia mara
kwa mara. Kwa hiyo hali hii inaweza kusababisha matatizo. Utumiaji wa dawa hii
inaweza kumweka mwananume pabaya kwa kutumia nguvu nyingi mpaka akapata na
matatizo ya msuli na mgongo kwa kuteleza kwa disc au pingili. Kuna hayo matatizo
hutokea baadae ya misuli kubana.
gkaijunga  - 9t food   |Registered |2009-12-20 09:09:41
Kila kitu kina faida na hasara zake, so watu wawe huru kuamua kutumia dawa hizi
au la. Binafsi nashauri mazoezi na matumizi ya asali kwa wenye matatizo ya aina
hii.
Wakoru  - Mkulima   |41.220.128.xxx |2010-01-06 06:30:11
I hope the most importsnt here is not the drus, ni lishe na utulivu wa mawazo
pamoja na kotokuwa na stress!!!
theo   |80.254.146.xxx |2010-02-18 04:35:46
kwani wadau hili tatizo huwa linasababishwa na nini??????mimi kama binti
nawaunga wadau mkono jamani inakera sana na ndio hatua ya kwanza inayofanya watu
watoke nje.......
i think tukijua source we can find solution sio kwa
kubahatisha mana matangazo ya dawa za aina iyo yapo mengi ila sioni mafanikio
yake.
Adonaya  - How do I get help!   |41.188.184.xxx |2010-03-07 00:48:40
I have read what you have given us on the medicine. So, how can I get? Tell me
please so that I can buy
mukulu wa nzukulu  - dawa za kuongeza ufanisi kitandani   |80.72.96.xxx |2010-03-26 02:24:59
ni tatizo kubwa kwa jamii yetu ya tz, sio kwamba kuwahi kufika ni lazima iwe
tatizo, inawezekana ukawa umempenda na kumtamani huyo girl kwa muda mrefu sana,
pia biological reasons,maumbile ya dada zetu,ujuzi n.k, also stress can lead to
this problem etc.
Aisee Bwashe  - Is it Available in Tanzania already?   |41.194.37.xxx |2010-04-14 02:19:44
Wadau naomba mnifahamishe kama tayari hii dawa ishafika nchini na ni maduka gani
yanauza?
Aisee Bwashe  - Hii dawa ipo wapi   |41.194.37.xxx |2010-04-14 02:25:44
Wadau niambieni hii dawa ishafika tanzania?
BLACKMANNEN   |194.237.142.xxx |2010-04-14 18:58:44
Watanzania wanapoletewa mada za ngono, huzichangamkia kweli kweli kuzichangia.
Angalia, hii ni mada ya siku nyingi zilizopita, lakini watu bado
wanachangia.

Kuna mada za AFYA na Chanjo ya HIV, wanazipita bila kuzichangia,
na inawezekana hawakuziona kabisa.

Watanzania kama tungechaguliwa kwenda
kuishi kwenye Bustani ya Eden, sidhani kama tungeweza kufuata masharti ya
kutokulila tunda la katikati ya Bustani.

This Is Black=Blackmannen
Mutta  - Je wewe si mtanzania?   |212.165.169.xxx |2010-04-19 06:02:28
Bwana BLACKMANNEN nafikiri nawe umetoa maoni yako kwenye blog hii, pia nadhani
nawe ni mtanzania, je nawe unapenda ngono? kama hupendi ulitakiwa usichangie
kabisa, kula tunda mkuu ni muhumu sana, hakuna asiyelipenda!
komba  - UFANISI KITANDANDANI   |41.191.92.xxx |2010-04-25 06:07:22
JEE UNAWASAIDIAJE WANAWAKE KUFURAHIA NA KUONGEZA UFANISI KITANDANI?
Festo Nyang'anyi  - Unajua wengine wanateswa na ndoa zao!   |196.201.151.xxx |2010-05-19 07:16:08
kama kweli hii dawa imepatikana basiu liwe sulihisho kwa wanaume waliowengi,
kwasababu, matatizo nkama yaha yapo kwa jamii, unajikuta mwanaume unalea mtoto
ambae sio wako kisa ufanisi mdogo mama katoka nje kutafuta ufanisi kwa mwanaume
mwingine.ila tuangalie upande wa pili wa madhara kila kitu kinachoingia ndani ya
mwili wa binadamu ni sumu na kina madhara ingawa yanachukuwa muda mrefu
kujitokeza. but tuwe nmakini kwa hili watanzania wenzagu. cha msingi tufanye
mazoezi na kupunguza msongo wa mawazo nafikiri tutafanikiwa kupunguza hili
tatizo.
Write comment
Name:
Email:
 
Title:
UBBCode:
[b] [i] [u] [url] [quote] [code] [img] 
 
 
Please input the anti-spam code that you can read in the image.

3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."

Habari Motomoto

  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20

Login Form