Saturday, July 31, 2010
   
Text Size

Tafuta kwenye Website hii

Henry Joseph Shindika aula

Aliyekuwa nahodha wa klabu ya simba nchini Tanzania hapo jana usiku alitambulishwa mbele ya mashabiki wasiopungua 5000 kwenye uwanja wa Gjemselund huko Norway.

Kocha mkuu wa klabu hiyo bwana Tom Nordile alisema kuwa anaamini nahodha huyo wa zamani wa simba ataisaidia timu yake mpya ya Kongsvinger kufanya vizuri kwenye ligi ya nchi hiyo.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Tanzania amekabidhiwa jezi namba 2 ikiwa ni wiki mbili tu tangu asaini mkataba ambao utamuingizia kitita cha shilingi miliono 260 kwa mwaka.

Comments
Add New Search
Deusdedith Kitambi  - Tanzania football fan   |213.136.112.xxx |2009-07-12 08:21:04
HONGERA HENRY HUO NI MWANZO MZURI KWA WATANZANIA, NAMTAKIA PIA NGASSA HERI.
Deusdedith Kitambi   |213.136.112.xxx |2009-07-12 08:22:13
HONGERA.
ELIARINGA E.MACHA  - SPAM   |41.222.60.xxx |2009-07-14 02:53:57
HONGERA SANA HENRY JOSEPHU (SHINDIKA)MAANA HAYO NI MAFANIKIO TOKA KWA TIMU YAKO
YA SIMBA NA TAIFA STAR.KEEP IT UP.
shabani  - Hongera   |41.204.128.xxx |2009-07-14 13:02:52
Mimi sio mpenzi wa Simba lakini nimefurahishwa na maendeleo ya mchezaji huyo
alikuwa klabu hiyo msimbazi,kwa kweli ni hatua nzuri kwa wachezaji wetu,natoa
mwito wengine wajitahidi ili wacheze huko Ulaya na kwingineko halafu waje
watusaidie kwenye timu ya Taifa.
keep it up!!!!!!!!!!!!
sostenes alto ndunguru  - Hongera Stars   |94.246.126.xxx |2009-07-15 02:43:46
Napenda kuipongeza Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kwa kuinyoa New
Zealand na hatimaye kuchupa hadi nafasi ya 97 katika FIFA Rankings. Sasa TFF
tunaomba mechi zaidi za timu kutoka nje ya Afrika!!!!!!!!!!!!!!!??!!!
sostenes alto ndunguru  - Hongera Real Madrid kwa usajili kabambe!   |94.246.126.xxx |2009-07-15 02:55:58
Napenda kuipongeza Real Madrid ya Hispania kwa kusajili viungo bora na forward
kali. Ushauri: Nikiwa shabiki wa Real nawashauri sasa wasajili beki kali kama
ya Chelsea ya uingereza. Wamgemsajili John Terry, Nemanja Vidic, Maicon wa
Brazil, Pia wamrejeshe kocha Vincent Del Bosque.
yusuph fido  - fidolas   |80.250.174.xxx |2009-08-01 02:45:56
sasa zile ndoto zetu za watanzania zinaanza kuonekana!!usemi ni ule ule tu
(samaki mmoja akioza wengine pia mule mule)hii inamanisha kuwa kama yeye kaanza
wengine watafuatia!!naipongeza taifa stars na simba kwa kuweka chini ushabiki wa
bongo usio na maana na kuangalia maendeleo ya timu yetu ya taifa!!mungu ibariki
tanzania mungu mbariki henry joseph .
Omar  - Hongera Henry Joseph   |213.100.49.xxx |2009-08-03 08:27:05
Huo ni mwanzo mzuri kwa wachezaji wa Tanzania. Hii inaonesha kwamba Tanzania pia
tunao wachezaji wazuri tu kucheza nje. Lakini pia tusisahau kwamba tunahitaji
wajenga msingi mzuri nyumbani ili Tanzania ijulikane katika ramani ya mpira kitu
ambacho kitarahisisha kwa wachezaji wetu kujulikana mara moja.
Omari   |86.96.227.xxx |2010-02-18 11:35:12
Kila kitu kina mwazo na huwo ndio mwazo
naamini wengi watafata HONGERA SANA
BWANA Henry Joseph,
mbonea mnzava  - mpenda pesa   |41.194.28.xxx |2010-07-17 02:16:52
hongera sana h. joseph na tunakutakia mafanikio zaidi ya hapo kaka na Mungu AWE
NAWE KATIKA timu yako mpya na usiisahau Taifa Stars itakapokuita usikatae kuja
kwa maana siku hizi kumetokea tabia ya wachezaji wengi wanaocheza mpira nje ya
nchi zao wakiitwa kuyachezea mataifa yao wanagoma. wewe usiwe hivyo kijana.
HONGERA SANA
Write comment
Name:
Email:
 
Title:
UBBCode:
[b] [i] [u] [url] [quote] [code] [img] 
 
 
Please input the anti-spam code that you can read in the image.

3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."

Habari Motomoto

  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20

Login Form