Saturday, July 31, 2010
   
Text Size

Tafuta kwenye Website hii

AFYA! AFYA! Mambo yote muhimu haya hapa

Majibu yote kuhusu afya yako hapa. Usiondoke kwenye mtandao huu bila kusoma habari hizi muhimu za afya yako. Hapa kuna maelezo ya kutosha kabisa ya kila aina ya ugonjwa na jinsi ya kuratibu magonjwa hayo. Pia tatizo kubwa la DEPRESION limeongelewa kwa undani.  read more......

Comments
Add New Search
Anonymous  - Hii ni nzuri sijawahi ona   |41.204.128.xxx |2009-08-30 14:08:26
Tz live news please endeleeni kutulutea mambo mazuri kama haya, maana mmnisaidia
mno ktk afya yangu
Mohammedy Jula  - Student   |196.46.109.xxx |2009-09-01 05:24:53
Mimi ni mwanafunzi wa kidato cha 5 katika shle ya sekondari tegeta.
Nauliza
kuhusu Ugonjwa wa sukari unasababishwa na nini?
nimeugua maradhi haya kwa miaka
miwili sasa lakina sikupata jua chanzo chake.
Namba msaada kwa hilo.
admin   |SAdministrator |2009-09-01 06:59:14
Ugonjwa wa kisukari upo wa aina mbili ,aina moja inasababishwa na kukosekana kwa
insulin ya kutosha mwili, insulin kazi yake nikubadili sukari ya ziada mwilini
na kuiweka katika hali ambayo mwili unaweza kuitunza bila kuleta madhara. yani
kitaalam insulin inabadili glocose kuwa glycogen.Aina hii ya kisukari sifahamu
sababu yake haswa , mi naichukulia kama ni ugonjwa ambao unatokana na asili. Na
aina nyingine ya kisukari ni ile inayosababishwa na na upungufu wa hormone
ambayo inasharabu maji katika viriba vya mkojo, hormone hii kitaalam huitwa anti
duratic hormone,mara nyingi watu wanaokumbwa na aina hii ya kisukari huwa ni
wale wanaotumia pombe, yani alcohol
LERUMBE  - Medical Officer   |196.43.74.xxx |2009-11-26 06:58:54
Kisukari ni ugonjwa utokanao na tatizo la mwili kumeng'enyua vyakula vya
aina ya wanga baada ya kufikia hatua ya sukari katika mchakato
wa kutengeneza nishati inayotakiwa kutumiwa na chembe hai za mwili.
Mwilini kuna tezi kubwa karibu kati ya tumbo kubwa na utumbo mwembamba
sehemu ya mwanzo au "Duodenum", nalo huitwa kongosho au
"Pancreas". Kwenye kongosho kuna vitezi vidogo viitwavyo Islets of
Langerhan ndivyo hutoa homoni iitwayo Insulin , nayo ndio kichocheo
cha chembe hai za mwili kuweza kujichotea sukari kutoka kwenye damu na
kuiunguza kupata nishati. Sasa: Kisukari ni ugonjwa utokanao na
mwili kushindwa kutumia sukari iliyo kwenye damu kwa sababu
mbalimbali: 1)Kutokuwapo kwa insulin mwilini kwa kuwa kongosho haitengenezi
2) Kuwapo kwa insulin ambayo ni kidogo mno kwa mahitaji ya mwili ya
sukari 3) Chembe hai za mwili k...
Anonymous   |41.204.128.xxx |2009-09-01 07:31:25
Ugonjwa wa sukari ya kupanda unasababishwa na kufail kwa kongosho linalotao
insulin hivyo kiasi cha insulini kinakuwa ni kidogo au hakuna kabisa sababu ya
kongosho failure
Mohammedy Jula   |196.46.109.xxx |2009-09-01 05:25:46
op;o
Anonymous   |81.199.176.xxx |2009-09-02 05:10:00
nataka nipunguze uzito nafanya nini?http://http://http://http://
Anonymous   |196.43.76.xxx |2009-09-02 09:37:15
Jibu hili hapahttp://www.webmd.com/diet/diet-health-check/def...
kester  - swali   |41.220.128.xxx |2009-09-23 03:58:18
Kwanza nashukuru Tz Live kwa kutuletea Mada hii.Swali:
Je kuna madhara ya aina
yoyote yanayoweza kutukumba sisi tunaopenda Kunywa KAHAWA?,Kwani mimi ni
miongoni mwa wanaopenda kunywa kahawa sana.Aksante!
Bakari Abedi  - swali   |196.43.79.xxx |2009-09-25 06:11:22
mimi ni mvulana wa miaka 26tatizo langu ni kwamba mimi ni muathirika wa HIV
nimesikia kuwa kuna dawa za kutibu ungonjwa huu je? ni kweli? naumiasana na
sijui hata ni vipinitawaelezawazazi wangu, nashindwa kufanya kazi kwasababu
hiinaomba msaada wenu.
Simon Okoka virumpu  - JE PROPOLIS INAWEZAJE KUONGEZA CD4 COUNT   |41.223.4.xxx |2009-09-26 15:53:38
MIE PIA NI MWATHIRIKA NAISHI KWA MATUMAINI, ILA NIMESIKIA KUWA PROPOLIS
INASAIDIA SANA KUONGEZA CD4, MIE NINAZO 620 NATAKA ZIWE 1500 HIVI.

KAMA
ZINAWEZA KUNISAIDIA ZINAPATIKANA WAPI HAPA TANZANIA? NA JE KUNA SUPPLEMENT GANI
NAWEZA TUMIA ILI KUKIDHI HAJA YANGU?
UMAGA  - KIKWAPA   |196.46.120.xxx |2009-12-16 01:13:53
Mimi nina tatizo la harufu ya kikwapa hata nioge vipi au nipake deodorant gani
hali ni ile ile nisaidie
ummy  - dawa ya kikwapa   |193.220.86.xxx |2009-12-23 00:38:26
kuna matibabu ya aina mbili ya asili ambayo yanasaidia sana tatizo hili.
1.
Tumia maji yaliyolowekewa sufuria la ugali,yachuje kisha yatumie kusafishia
mwili wako mzima(ogea).
2. Jisugue kwapani kwa kipande cha ndimu kila siku
asubuhi na jioni baada ya kuoga.

Usipende kujipulizia parfum au deodorant
mara kwa mara hasa ukiwa haujaoga kwani nayo pia huchangia tatizo la kunuka.
Mama rose  - kuwashwa   |196.44.161.xxx |2010-01-15 00:56:56
Mimi naomba unisaidie nina ugonjwa wa kuwashwa mwili mzima na nikianza kuwashwa
koo linawasha na ninakooa sana hadi natamani kutapika, pia kunuka sana mdomo
hadi naona aibu ya kuongea na wenzangu kwa kutawaona wanakimbiza uso. Basi
nasikitika sana.

naomba ushauri wako
asante
Mama rose   |196.44.161.xxx |2010-01-15 01:17:09
Ninaomba unisaidie. Tatizo langu ni kuwashwa sehemu za siri. nimetumia sana dawa
hadi nimeenda kupima HIV kama mara kumi hivi na zaidi kwa kuwa kipindi
ninawashwa hadi ninaota vipele nikaenda kupima kwa kuwa ilikuwa kama dalili za
HIV. Kwa bahati nikakutwa sina. naomba unisaidie ili nijue nifanye nini.
ASHURA MPEMBA  - UTI   |196.201.151.xxx |2010-03-17 08:39:32
Mtoto wangu anasumbuliwa sana na ugonjwa wa U.T.I(uchafu kwenye mkojo)na
ametumia sana antibiotic lakini bado tatizo lipo palepale, maji anakunywa kwa
wingi na usafi wa nguo najitahiji sana kumtunza. Pia hata kipimo cha culture
amefanyiwa na dawa alishatumia baada ya culture lkn bado anasumbuliwa. Je
nifanyeje? anaumli wa miaka 2. Naomba msaada.
zionbouy  - Babuu   |196.46.109.xxx |2010-07-29 03:47:47
Nina tatizo moja kubwa sana la ulevi wa pombe kupita kiasi na uvutaji wa sigara
kitu ambacho naona kinanitesa sana katika maisha yangu..usiku sipati usingizi
bila pombe chakula hamu sina maendeleo yangu kikazi yanazorota siku hadi siku
najitahidi sana kupambana na hali hii lakini naona imenitawala na mpaka uchumi
wangu kama nimewekeza kwenye anasa. Naomba ushauri wako au kama ni tiba ya hili
tatizo niondokane na hili janga linaloniandama.
Write comment
Name:
Email:
 
Title:
UBBCode:
[b] [i] [u] [url] [quote] [code] [img] 
 
 
Please input the anti-spam code that you can read in the image.

3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."

Habari Motomoto

  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20

Login Form