Saturday, July 31, 2010
   
Text Size

Tafuta kwenye Website hii

Wanafunzi walioteketea kuzikwa kaburi moja leo

WAKATI mazishi ya miili ya wanafunzi 12 yanafanyika leo katika kaburi moja, serikali imetangaza kuifunga Shule ya Sekondari Idodi mkoani Iringa kwa siku 21 kuanzia juzi.

Uamuzi huo wa serikali ulitangazwa jana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe, ikiwa ni siku mbili baada ya janga la moto kutokea shuleni hapo na kuua wanafunzi 12, kuteketeza bweni na kusababisha hasara ya zaidi ya sh milioni 105.

Maghembe ambaye anatarajia kushiriki katika mazishi hayo shuleni hapo, alisema serikali bado inatafakari juu ya kukabiliana na majanga ya moto katika mabweni ya wanafunzi wa shule za sekondari nchini.

Alisema Waziri Mkuu Mizengo Pinda, anatarajiwa kuongoza mazishi ya wanafunzi hao.

Aidha, ofisi yake kupitia kitengo cha maafa imetoa rambirambi ya sh milioni 22.

Hata hivyo, wadau mbalimbali wameanza kutoa misaada yao kwa shule hiyo ikiwemo Kampuni ya Asas Iringa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa, Ledian Mng’ong’o (CCM).

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mohamed Abdulaziz alimweleza mwandishi wa habari hizi jana kuwa tayari Kamati ya Maafa ya Mkoa wa Iringa imeanza kupokea misaada mbalimbali kutoka kwa wadau hapa nchini.

Alisema misaada iliyopokelewa hadi juzi jioni ni magodoro 159, mablanketi 80, ndoo 50 na kanga doti 126 vyote vikiwa na thamani ya sh 4,032,000 kutoka Kampuni ya Asas.

Nayo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa, ilitoa mashuka 105 yenye thamani ya sh 420,000 na Mfuko wa Pesheni Taifa (PSPF) uliotoa mashuka 100 yenye thamani ya sh 400,000.

Wengine ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Iringa Mjini, Abed Kiponza aliyechangia magodoro 16, mablanketi 56, ndoo saba, vikombe vya kunywea maji vitano na galoni moja vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya sh 500,000.

Naye Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa, Mng’ong’o alitoa kanga doti 100 zikiwa na thamani ya sh 320,000 ambapo jumla ya misaada yote iliyopokelewa ni sh 7,846,500.

Abdulaziz alisema misaada hiyo ilikabidhiwa juzi usiku kwa wanafunzi chini ya uangalizi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama.

Kwa upande wake, Mkuu wa Shule hiyo, Raymond Mlasu, alisema wanafunzi wa kike wanaohitaji msaada baada ya vitu vyao kuteketea kwa moto ni zaidi ya 400.

Alisema shule hiyo yenye kidato cha kwanza hadi cha nne, ina jumla ya wanafunzi 1,045, wakiwemo wavulana 561 na wasichana 484 huku wanafunzi wa bweni wakiwa 911.

Hata hivyo, mkuu huyo alisisitiza kuwa chanzo cha moto huo ni mshumaa uliokuwa umeachwa bila kuzimwa na mwanafunzi aliyekuwa anasoma na kupitiwa na usingizi.

Abdulaziz alikanusha na kusema moto huo si hujuma kama ambavyo moja kati ya magazeti ya kila siku (si Tanzania Daima) hapa nchini yalivyoandika jana.

Wakati huo huo, Mjumbe wa Bodi ya shule hiyo, Salum Chota, alisema alikuwa wa kwanza kufika eneo la tukio kuzima moto huo.

Chota alisema uvumi wa kuwa mwanamama mmoja alikuwa akiwazuia wanafunzi kupita mlangoni si kweli, kwani mtu aliyekuwa mlangoni ni mwanafunzi wa kiume ambaye alikuwa akisaidia kuwaokoa wahanga wa tukio hilo.

Alisema ugumu wa wanafunzi hao kutoka katika bweni hilo ulitokana na nondo zilizowekwa katika bweni hilo, hivyo wananchi kulazimika kuvunja madirisha na kubomoa milango ili kuweza kuokoa wanafunzi hao.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Iringa, Dk. Ezekiel Mpuya, alisema hali za majeruhi wa tukio hilo zinaendelea vizuri ukilinganisha na juzi walipofikishwa hospitalini hapo.

Mkuu wa Mkoa, alisema kuwa pamoja na maiti moja kati ya 12 kutambuliwa na ndugu, bado wazazi wote wa wanafunzi waliokufa katika tukio hilo walikubaliana maiti zote kuzikwa katika kaburi moja shuleni hapo.

Wanafunzi waliokufa katika tukio hilo ambao leo watazikwa kaburi moja ni Matrida Mtewele, Adelvina Kwama na Elizaberth Mtavila waliokuwa wanasoma kidato cha kwanza.

Wengine ni Digna Nduguru, Chake Kuyaa, Seciliana John, Lazia Kihwele, Witness Mbilinyi na Stellah Mwigavilo waliokuwa wanasoma kidato cha pili.

Pia wamo Falha Abdallah na Jesca Wissa waliokuwa kidato cha tatu na Maria Ndole wa kidato cha nne ambapo alisema kutokana na marehemu hao kuteketea kiasi cha kutotambulika, wametumia njia zingine kupata majina yao.

Majeruhi waliolazwa hospitalini ni Mwizarubi Eliasi, Lucy Sawani, Faraja Sodike, Anoda Ambali, Lela Mkuya, Prisca Melele, Evamary Carlos na Sabrina Abdulhaman.

Wengine ni Lenna Barugu, Zuhra Mazora, Veronika Nyamule, Theresia Zuvapi, Esther Zayumba, Ando Mamba, Irene Mponzi, Ares Ndaga, Lucy Luvanda, Upendo Nyamadule, Fraja Palinoo na Helena Mapunda.

Comments
Add New Search
furaha  - bweni lililoungua na moto   |196.44.165.xxx |2009-08-25 01:45:00
kwanza kabisa nawapa pole wazazi, ndugu na watanzania kwa ujumla kwa janga hili
la moto, kiukweli inatisha sana.
ushauri wangu ni kwa hawa wasanifu wa majengo,
naomba wajitahidi kuweka milango mingi ya dharura, na pia ningeshauri bweni
lisiwe kubwa kama hili liwe la kawaida lenye partition ya kubeba angalau
wanafunzi hata 30/40 ili kuweza kuondoa madhara zaidi. Mungu azilaze ROHO za
Marehemu mahala pema peponi AMINA.
Nana  - Ni Janga la kitaifa   |78.41.227.xxx |2009-08-25 04:54:08
Kwa kweli hili ni janga la kitaifa - kuna mambo mengi ya kijufunza hapo ili
kuweza kuepukana na majanga ya aina hii! Je tupo tayari kweli kujifunza au ni
kusema na kusahau?
Futeh A.  - Mfanyakazi   |41.221.35.xxx |2009-08-25 09:19:24
Ingawa in wakati mgumu hasa kwa ndugu zangu kule Iringa kupokea msiba huu
mkubwa, ukweli ni kwamba si jambo jepesi hasa unpofiwa na binti yako au mvulana
wako ambae ulikuwa na mategemeo makubwa kwake. Ni lazima sote tushikamane lakini
huku tukiiomba serikali kuchunguza kwa makini chanzo cha ajali ili kuepusha
ajali nyingine katika shule za sekondari zinazotokea kwa mfululizo. Shule
binafsi lazima zikidhi masharti (standards) yanayowekwa na serikali na pia
serikali lazima izisimamie shule hizi kwa umakini mkuu si kuruhusu shule
kuanzishwa kiholela hata kama ni katika nia njema ya kuwasaidia watoto wa walala
hoi vijijini. Mungu azewake roho za marehemu peponi. Bwana alitoa na Bwana
ametwaa jina lake lihimidiwe. Hivi ndivyo tunavyoweza kusema hatimae hatuna
uwezo zaidi.
NASHON  - mzalendo   |196.201.151.xxx |2009-08-26 00:41:40
Natoa lawama zanngu kwa serikali hasa hili la kukosekana kwa umeme katika shule
za sekondari
huu ni uzembe usiovumilika nahisi viongozi wa serikali hawako
sahihi kutoa rambi rambi wakati wao ndio chanzo kwa kushindwa kuzipa shule umeme
wakati ni huduma za msingi
hiviwanafunzi wanasoma vipi? POLENI NDUGU ZANGU
WATANZANIA MASKINI WENZANGU KWA MSIBA ULIOTUKUTA. BWANA ALITOA NA BWANA AMETOA
JINA LAKE LIHIMIDIWE AMEN
Anonymous   |196.201.151.xxx |2010-01-15 00:48:19
Ni janga la Kitaifa.
Napenda kutoa pole kwa Ndugu zangu wa Iringa na WaTanzania
wote kwani hao waliokufa walikuwa viongozi watarajiwa wa Taifa hili.
Viongozi
wa Serikali ni lazima wafike mahala pa kuwa na hata ka chembe ka ubnadam kwani
shule nyingi hapa Tanzania hazina umeme na wanafunzi hawa wanatakiwa kushinda
mitihan,watasomaje???
Majanga ya moto yamezidi hapa Tanzania,sijui ni hatua
gani serikali imeshachukua lakini na dhan ni vema shule zikiwekewa FIRE
EXTINGUISHER na wanafuzi wapewe training jinsi ya kuzitumia kama mbinu ya
kuwaokoa watoto wetu pale linapotokea janga kama hili maana hata umeme unaweza
kulipuka.
SERIKALI MNAKAZI KUBWA YA KUFANYA JAPO MNAJIFANYA HAMZION,
Beatrice Zegera  - its time for action first   |196.44.161.xxx |2010-06-17 13:18:20
very sorry for the death of our beloved one, i think the Government can learn
through this do not wait until things happen to take action.but it is better to
take precaution before, because this is not the first time to lost students
particularly from Government schools.
ANGELA  - mwanafunzi TIA dar   |196.41.39.xxx |2010-07-13 06:02:47
dah! inaumiza sana jamani tumuombe Mungu awatie nguvu wafiwa,poleni sana
jamani,yatupasa kuwa makini zaidi katika majengo yetu jamani,pia serikali
tunaomba muangalie zaid katika swala zima la wanafuzi kwani mazingira mazuri
yanamsaidia mwanafunzi katika kusoma ,serikali iangalie pia kwa familia hizo
ambozo wamepata matatizo kwa sasa namna ya kuwasaidia
ANGELA   |196.41.39.xxx |2010-07-13 06:05:21
poleni sana wafiwa Mungu wa mbinguni awatie nguvu,jamani serikali na sisi
wananchi kwa ujumla tujitoe katika kusaidia maendeleo ya shule zetu,ona majanga
ya moto yanavyoteketeza ndugu zetu ni jukum la kila mmja jamani
Write comment
Name:
Email:
 
Title:
UBBCode:
[b] [i] [u] [url] [quote] [code] [img] 
 
 
Please input the anti-spam code that you can read in the image.

3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."

Habari Motomoto

  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20

Login Form