Saturday, July 31, 2010
   
Text Size

Tafuta kwenye Website hii

***BREAKING NEWS: Watuhumiwa wote kesi ya ZOMBE waachiliwa huru!!!***

Jaji Kiongozi, Salum Masati, wa Mahakama Kuu ya Tanzania akisoma hukumu leo iliyochukuwa masaa sita, amewaachia huru washtakiwa wote wa kesi hiyo ya mauaji.

Katika kesi hiyo, Zombe na wenzake walikuwa wakituhumiwa kuwaua wafanya biashara wa madini Ephraim Sabinus Chigumbi, Sabinus Chigumbi (Jongo), Mathias Lung’ombe na Juma Ndugu aliyekuwa dereva teksi na mkazi wa Manzese Dar es Salaam, Januari 14, mwaka 2006 katika msitu wa Pande, Mbezi Luisi wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Akisoma hukumu hiyo leo Jaji Masati alisema kuwa washtakiwa wote hawana hatia kwakuwa hakuna ushahidi wa moja kwa moja unaonesha kuwa watuhumiwa hao walihusika katika kufanya mauaji ya wafanyabiashara hao.

Jaji Masati amesema kuwa amekosa ushahidi wa kuwatia hatiani pamoja na kusikilizwa kwa mashahidi wote 37.

Katika kesi hiyo iliyosikilizwa zaidi ya miaka miwili, jumla ya mashahidi 37 walifika mahakamani katika siku tofauti tofauti kutoa ushahidi juu ya mauaji hayo.

Washtakiwa katika kesi hiyo walikuwa ni Abdallah Zombe ambaye alikuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam, Bageni, Makele, WP 4513 Jane, D1406 Mabula, D8289 Michael, D2300 Abeneth, B1321 Rashid, D4656 Rajab na D1367 Philipo.

Mshitakiwa Lema alifutiwa kesi baada ya kufariki dunia kutokana na kusumbuliwa na maradhi akiwa gerezani ambapo alilazwa katika Hospitali ya Saratani ya Ocean Road.

Baada ya kusomwa kwa hukumu hiyo baadhi ya mamia ya watu waliojazana ndani na nje ya mahakama walionekana kutoridhishwa na hukumu hiyo.

Mtuhumiwa pekee wa kike katika kesi hiyo WP 4513 Jane, alizirai baada ya hukumu ya kesi hiyo kusomwa , hivyo kufanya apakizwe kwenye gari la wagonjwa "ambulance" na kukimbizwa hospitali kwa ajili ya kupata huduma ya kwanza.

PICHA HIZI HAPA

zombe na wenzake walivyochomoa leo


ni kicheko wakati ACP Abdallah Zombe na wenzie wakiwa wamezungukwa na makachero na wanahabari wanaondoka mahakama kuu kupitia mlango wa nyuma mara baada ya mahakama kuwaona hawana hatia kwa mashitaka ya mauaji ya wafanyabiashara wa mahenge baada ya upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha tuhuma hizo

 


umati mkuwa wa wadau ulijaa hadi nje ya jengo la mahakama kuu



wakili machachari aliyemtetea zombe Mh. Jerome Msemwa, akipewa hongera wakati yeye na timu yake wakiondoka mahakama kuu baada ya kuigalagaza timu ya upande wa mashitaka

 


washtakiwa wakiwahi kudandia farasi mweupe baada ya kuchoropoka

 


wahi wahi afande.....

 


zombe akidandia vitara iliyokuja kumchukua

 


wadau wakiwa wameachiwa vumbi na vitara aliyopanda zombe

 


mahakama kuu palikuwa hapatoshi



zombe huyoooo anakitoa huku mashabiki
wake wakiimba zombe! zombe! zombe!!



Wakili wa Upande wa Serikali Jasson Kashozi akihojiwa na wanahabari mwara baada ya hukumu ya Zombe na waenzake 9 ambao wameachiwa huru na mahakama kuu baada ya kutopatikana na hatia jioni hii kutokana na mashitaka ya mauaji ya wafanyabiashara watatu iliyokuwa ikiwakabili.
Comments
Add New Search
ros  - Not fair   |196.46.109.xxx |2009-08-17 07:37:04
Cjafurahishwa na maamuzi ya mahakama hiyo for sure we are useless pple in this
world if u got no name or money!
ros  - NOT FAIR   |196.46.109.xxx |2009-08-17 07:38:51
Sio fair hata kidogo na wala cjafurahishwa na maamuzi hayo ya mahakama coz it
showz us pple with nothing we are useless kabisaaaaaaaaaaaaaa!
osmund  - mmh!   |81.199.160.xxx |2009-08-17 08:07:15
Ama kweli hii ndo Tanzania!zaidi na unavyoijua wewe na wanoijua wanasema nyamaza
kijana! hii ndo hukumu ya pirato yenyewe!
Amani  - muix   |41.220.128.xxx |2009-08-17 08:16:28
Zombe umeachiwa huru lakini kumbuka mbinguni unakesi ya kujibu kutoa nafsi ya
watu wasio na hatia.
ESHMAEL  - ndo hivyo!!!!!!!!!   |41.188.140.xxx |2009-08-17 08:22:18
thats itnowdays someone can do what he/she wants and get away with it!!!!
flein  - This is CCM!   |196.46.109.xxx |2009-08-17 08:31:09
Lazima mujue kwamba CCM inatumia vyombo vya ulinzi kufanya mambo yake, hivyo
mlikuwa mnategemea kabisa kuwa wangemwacha zombe afe kivyake??mbona
hawakumkamata mahita japo alikuwa na kashfa?basi kama tunashangaa hili la zombe
tusubiri la mramba na yona tutalia.
triple xxx  - Business Man   |193.134.242.xxx |2009-08-17 08:33:43
Angalieni sana 2010 msichague rangi, chama wala mtu....fanyeni uamuzi wa busara
kwenye uchaguzi ujao tuwapige chini ndugu zangu vinginevyo tumekwisha. Hao wote
washakuwa maharamia. Wanajuana na wanalindana na wako wanachukua vyao mapema.
Hakuna kiongozi yeyote wa serikali ya kijani atakuwa na kesi alafu ashindwe
mahakamani, maana hakimu au jaji anaambiwa hukumu hivi basi hakuna swali....
vmwenda   |196.43.64.xxx |2009-08-17 08:48:44
we cant say more but what l can see is not right and unfair.we have to live it
to our almight God.he will raise up his hand
mkereketwa   |41.223.228.xxx |2009-08-17 09:34:57
sijafurahishwa kabisa na hukumu iliyutolewa. hata ambao hawajui sheria
wanafahamu kuwa kilichotndeka sio sawa kabisa. Mahakama haiwezi kuwaachia watu
wote. Kwenye sheria hata kama kukutenda kosa kwa mkono wako lakini ulisaidia kwa
namna moja au nyingine kufanyika kosa unakuwa criminal liable. sasa hata wale
maaskari walioenda msitu wa pande hawana hatia? sio sawa kabisaaaaaaaaa.

Jamani serikali ingilieni kati hili swala.
laurian francis  - mfanyabiashara   |41.191.92.xxx |2009-08-17 09:40:06
SIAMINI KAMA ZOMBE KAACHIWA HURU,DUU HII NDIO BONGO.MAMBO VULULUVULULU
HAYAELEWEKI
NURU HEMED  - student   |41.191.92.xxx |2009-08-17 09:43:23
Tanzania inapoelekea ni kubaya, Zombe hakua wa kuachiwa huru. kweli money ni
kila kitu.
Mwananchi mwenye hasira  - Aiiibu jaji Masati   |133.51.84.xxx |2009-08-17 09:45:43
Kwa maelezo ya huku hii jaji Masati anataka kuwaambia Watanzania kwamba hakuna
mtu aliyeuawa, na hivyo hii ilikuwa kesi ya kughushi? Aangalie damu ya watu hawa
wasio hatia inaingia katika mikono yake! Busara imekosekana!
Brown  - Sio fair   |84.73.219.xxx |2009-08-17 10:38:12
Tuangalie Watanzania kama tutaendelea na mambo hayo, Dunia sasa imekuwa ni ndoga
sana kama kijiji, Tuangalia tusije tukachagua viongozi waotuua masikin alafu
tuna umizwa na sheria zetu wenyewe.
mwananchi mwenye hasira   |196.46.106.xxx |2009-08-17 12:16:25
its true all human being are equal but others are more equal than
others!!!!!!!!!!it real pain!!!!!!!!i' ll never vote 4 ccm!!!!!!!!!!!!!!!!MR
ZOMBE where is Ditopile?
john  - lawyers daaa!!!!!   |41.191.92.xxx |2009-08-17 12:32:23
me bwana i can't argue saaana, maana hili swala la zombe ni l kisheria zaidi,
lakini tukiangalia kwa mapana na marefu the case ended disappointingly, most of
us wanted the guys to pay for we did. but at the end of the day God ndo
mwamuzi/judge wa mwisho, EVERYONE SHOULD UNDERSTAND THIS!
john  - Lawyers daaa!!!   |41.191.92.xxx |2009-08-17 12:34:43
sorry, the second last line i meant" most of us wanted to see the guys pay
for what they did"
Mtanzania  - JIULIZE MBONA WOTE JELA NIMASKINI   |41.223.4.xxx |2009-08-17 13:11:33
ama kweli ndio maana bushoke aliimba "jiulize kwanini wote walio jela ni
maskini" Yaani nchi yetu niwataalam wa kuwatia hatiani wanyonge ila wauaji
na mafisadi wanaonekana hawana hatia. WATANZANIA TUAMKE NAKUPINGA HALI HII LA
SIVYO TUTAKUWA TUNAUWAWA KAMA SISIMIZI NA WENYE NACHO. WANASHERIA MNATUTIA AIBU
KUTETEA YOYOTE ILAMRADI ANAELA. UYO ZOMBE DAWA YUKE NIKUMUUKUMU KWA MIKONO YETU
TU
Lawyer  - Fair comment   |94.246.126.xxx |2009-08-17 23:39:40
To me it was fair as far as justice is concerned,siku zote upande wa mashtaka
unatakiwa kuprove case beyond a reasonable doubt kitu ambacho hakikufanyika
ipasavyo,mashahidi wameshindwa kuthibitisha hatia ya washtakiwa kwani hakuna
hata mmoja alieprove kuwa jamaa walihusika kwenye actual killing (Murder) kama
walivyoshtakiwa,inawezekana kuwa walihusika in one way or another,bt hiyo lazima
ithibitike pasipo kuacha mashaka,wangeweza kuwa accessories after the fact
lakini hii ni separate offence ambayo ingekuwa vyema kama ingekuwepo kwenye hati
ya mashtaka,Jaji asingeweza kuwahukumu kwa hiyo kwani sio kosa waliloshtakiwa
nalo.
Hakuna haja ya kunyoosheana vidole,Jaji kafanya kazi yake,ambae
hajaridhika Mahakama ya Rufaa ipo kwa ajili yake.
MWISHO NI LAZIMA TUJIULIZE
WALE MAREHEMU WALIUWAWA NA NANI NA KATIKA MAZINGIRA GANI,UTATA BADO UMEGUBIKA
SUALA HILI..
MSOMI  - TANZANIA NAYO SASA IN WASOMI   |41.138.192.xxx |2009-08-18 01:35:49
kwa kweli kwa mahamuzi ya case ya zombe imeionyesha tanzania kuwa nayo sas
imefika mahala pa kujivunia kuwa ina "lerned Brothers and sisters" tena
wenye busara na wanaofanya mahamuzi kwa misingi ya sheria na sheria peke yake
bila rushwa, uccm, wala mawazo na fikra dhanifu na bunifu za watu. Majaji na
mawakili hongereni sana endeleeni na moyo huohuo mungu awape utaalam na ufanisi
zaidi.
bint  - ulitegemea nin?   |196.43.79.xxx |2009-08-18 01:40:02
hivi mlitegemea nin wakat wale washitakiwa ndio mashahidi wa mauaji ,wao ndio
walio kamata hao wafanyabiashara na ndio wanaojua nin kilichotokea,wengine wote
walituzuga tu.
Kachalaaaa  - Uuuuwiiiii Mungu yupo   |196.1.52.xxx |2009-08-19 08:14:53
Hamna kitu hapo wala hakuna sheri a hapo haki sawa kwa wote ipo wapi Azimio la
Arusha? Kwa kweli sasa Police watatumaliza kama wameua Arusha, Dar, Mbeya and so
on wakamwachia Kombe that is not fairrrrrrr Hakuna ukweli kwenye hii Nchi Jk ni
hay kweli ulituomba kura zetu tukupigie?????
think big  - dr   |68.34.118.xxx |2009-11-19 11:30:50
haya maamuzi ya mahaka sio ya kweli kabisa haki tanzania haipo
Relief  - THIS IS IT   |196.41.62.xxx |2010-07-30 00:24:38
My dear brothers and sisters, tulilolingoja sasa limefika, we are at the vedge
of no return. God help us!!
Write comment
Name:
Email:
 
Title:
UBBCode:
[b] [i] [u] [url] [quote] [code] [img] 
 
 
Please input the anti-spam code that you can read in the image.

3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."

Habari Motomoto

  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20

Login Form