Waasi 90 wa FDLR wauawawa Kongo
Thursday, 11 March 2010 06:52
Wanajeshi wa serikali walioko eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo wamewauawa waasi 90 wa Kihutu tangu walipoanzisha mwezi uliopita operesheni mpya ya kuwafurusha. Kwa mujibu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUC,


Polisi wa Ireland wamewakamata watu 7 wanaotuhumiwa kuhusika na njama ya kumuua mchora vibonzo mmoja wa Uswisi.Mchoraji huyo wa gazeti alichora kibonzo cha Mtume Muhammad S.A.W. akiwa na mwili wa mbwa.
Kiasi cha wanaharakati alfu 5 wameandamana hii leo ili kulishinikiza baraza la mawaziri kujiuzulu pamoja na kumtaka Rais Umar Yar'Adua anayeugua awahutubie wananchi.Ni wiki mbili tangu kiongozi huyo arejee nchini baada ya kutibiwa nchini Saudi
Mkuu wa sera za Umoja wa Ulaya Catherine Ashton ameulaani uamuzi wa Israel wa kuendelea kuyajenga makazi 1600 mapya katika eneo la Jerusalem Mashariki la Waarabu wengi. Kauli hizo zimetolewa baada ya Makamu wa
Polisi wa kupambana na ghasia nchini Togo wamelazimika kutumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji zaidi ya 1,000 waliokuwa wamekusanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo, Lome, kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais.
Kamanda wa ngazi ya juu wa kundi la wapiganaji wa kiislamu la Hizbul Islam nchini Somalia, Bare Ali Bare, amepigwa risasi na kuuwawa mjini Mogadishu hii leo. Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo, mtu asiyejulikana aliyekuwa
Waziri mkuu wa Ugiriki, George Papandreou, anatarajiwa kukutana na rais wa Marekani Barack Obama mjini Washington hii leo. Mkutano kati ya viongozi hao unafanyika wakati kukiwa na wasiwasi kwamba walanguzi wa fedha wanahujumu juhudi za Ugiriki
Marekani na mashirika ya kutetea haki za binadamu yameitaka Nigeria iyachunguze kwa uangalifu mauaji ya watu takriban 400 waliouwawa wakati wafugaji Waislamu walipovivamia vijiji vya Wakristo karibu na mji wa Jos,
Utawala wa kijeshi nchini Niger umemuachilia huru Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo, Ali Badjo Gamatie na mawaziri wanne, lakini bado unamshikilia Rais wa zamani Mamadou Tandja. Utawala huo wa kijeshi uliomuondoa madarakani Rais Tandja Februari 18 mwaka
Rais wa Misri, Hosni Mubarak leo anatarajiwa kufanyiwa upasuaji katika kibofu cha nyongo.
Waziri Mkuu wa Uingereza, Gordon Brown ametetea hatua ya nchi hiyo kushiriki katika vita vya Iraq. Bwana Brown amesema anaamini ilikuwa halali na ilifanya hivyo kwa sababu zilizo sahihi.
Waziri Mkuu wa Ugiriki, George Papandreou amekutana na Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel mjini Berlin kujadili mipango ya Ugiriki ya kukabiliana na mzozo wa bajeti yake. Katika mkutano wa pamoja na waandishi habari, Bibi Merkel alisema katika mazungumzo
Nchini Ivory Coast, upande wa upinzani umetoa majina ya mawaziri 11 katika serikali mpya ya umoja wa taifa. Serikali hiyo iliyotangazwa juma lililopita, ina mawaziri 16 kutoka chama cha FPI
Mvua kubwa zilizonyesha mashariki ya Uganda zimesababisha mafuriko na zinazuia kazi za uokozi katika eneo ambako nyumba zimegubikwa na maporomoko ya udongo. Kwa mujibu wa kamanda wa polisi wa eneo hilo la
Bunge la Ugiriki leo linapiga kura kuidhinisha mpango uliopendekezwa na serikali katika jitahada za kupunguza gharama zake kwa hadi Euro bilioni 4.8. Serikali inachukua hatua hizo ili
Katika kesi kubwa kabisa ya ugaidi nchini Ujerumani, watu wanne waliokiri kupanga kuripua vituo vya kijeshi vya Marekani viliopo Ujerumani, wamehukumiwa vifungo vya jela vya hadi miaka 12.
Serikali ya Waziri Mkuu wa Ukraine, Yulia Tymoshenko imevunjwa ikiwa ni mwezi mmoja baada ya kushindwa katika uchaguzi wa urais nchini humo.
Waziri Mkuu wa Ugiriki, George Papandreou, ameonya kuwa nchi yake iko katika hatari ya kufilisika, kama haitachukua hatua madhubuti za kutatua mzozo wake wa kifedha.
Rais Michelle Bachelet wa Chile, amesema idadi ya watu waliouawa na tetemeko la ardhi lililotokea nchini humo mwishoni mwa wiki iliyopita, imeongezeka na kufikia 795. Kufuatia uporaji ulioenea, Rais Bachelet ameamuru wanajeshi 11,000 kupelekwa katika
Mahakama kuu nchini Ujerumani imebatilisha sheria ya Umoja wa Ulaya kuhusu uhifadhi wa data za mawasiliano. Sheria hiyo ilitaka kuhifadhiwa kwa mawasiliano ya simu na mtandao kwa muda wa miezi sita.
Venezuela imetupilia mbali mashitaka yaliyotolewa na jaji wa Uhispania kuwa ilishirikiana na makundi ya waasi ya Colombia na Basque kupanga mauaji ya rais wa Colombia. Wizara ya mambo ya nchi za nje ya Venezuela